SERIKALI IMETAKIWA KUHARAKISHA MBEGU NA MBOLEA ZA RUZUKU KUFIKA KWA WAKATI MAENEO HUSIKA

                      

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida MARTHA MLATA ameiomba serikali kuharakisha wakulima wa mkoa huo wanafikiwa na mbegu na mbolea za Ruzuku kwa wakati ili kuwawezesha wakulima kulima kwa tija na kuzalisha mazao mengi.


MLATA alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Manispaa ya Singida katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. EMMANUEL NCHIMBI akiwa katika Ziara yake ya kuimarisha Chama, kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwaanda wananchi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Alisema kumekuwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa Mbegu za Ruzuku kuwafikia wakulima, ambayo inasababisha wakulima kuchelewa kulima kwa wakati kwa kusubiri Mbegu hizo.

                           
Aidha MLATA aliongeza kuwa kuna ucheleweshwaji wa Mbolea za Kupandia na Kukuzia hivyo kusababisha Wakulima kuendelea kulima kienyeji na kuvuna mazao kidogo na yasiyo na tija.

Hivyo aliomba serikali kuhakikisha Mbegu na Mbolea za Ruzuku zinawafikia wakulima kwa wakati sahihi ili waweze kuzalisha kwa tija na waweze kuinua vipato vyao.

                              
Kwa upande wake MNEC wa Mkoa wa Singida YOHANA MSITA aliiomba Serikali kujenga miundombinu mizuri ya Soko la Vitunguu ili kuwawezesha Wafanyabishara na Wakulima kufanya Biashara kwenye mazingira mazuri.

MSITA alisema Soko hilo la Vitunguu linasaidia kutoa ajira kwa wakazi wa Mkoa wa Singida na mikoa jirani ambapo hujipatia vipato kwa familia zao kutokana na shughuli mbalimbali zinazofanyika hapo.

Aidha MSITA alisema Soko hilo la Vitunguu pia linachangia Pato la Taifa kutokana na Ushuru na Tozo mbalimbali zinazokusanywa katika Soko hilo kwa Vitunguu vinavyotoka sokoni hapo hupelekwa hadi nchi jirani za Uganda, Burundi, Jamuhuri ya Congo na nchi nyingine.
                              

Hivyo alisema kutokana na Miundombinu ya Soko hilo kuwa sio mizuri kwa wafanyabishara na wakulima wanaoleta mazao yao, Serikali ione umuhimu wa kuboresha Miundombinu hiyo ili kuvutia wafanyabishara wengi katika soko hilo ili serikali iweze kukusanya Mapato mengi.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments