Ubovu wa barabara wamliza muwakilishi Ulanga

ULANGA, Morogoro: MBUNGE wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham ameiomba serikali kusimama na wananchi wa jimbo hilo katika kipindi cha mvua inayosababisha kuharibika kwa miundombinu ya barabara.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham

Akizungumza na HabariLEO, mbunge huyo amesema kilio kikubwa cha wananchi ni ubovu wa barabara ambazo zimeharibiwa na mvua licha ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika (TANROADS) lakini hakuna utekelezaji wowote.

Amesema Serikali kupitia wakala ya barabara TANROADS imekuwa ikipeleka wakandarasi wasio na uwezo wa kufanya kazi hizo ikiwemo mkandarasi kutokuwa na vifaa maalumu kwa ajili ya kuendeleza uboreshaji wa barabara hizo.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hizo, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Kyamba Alinanuswe amekiri kuwepo wa hali hiyo huku akisema kuwa sababu kubwa iliyosababisha kuchelewa matengenezo ya barabara ni mvua zinazoendelea kunyesha hata hivyo matengenezo yameanza.

Aidha meneja huyo amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha zimetajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa barabara hizo hàta hivyo Tanroads itahikisha inafika na kurekebisha barabara hizo licha ya kukiri kuchelewa kuanza kazi hapo awali.

Jimbo la Ulanga ni miongoni mwa majimbo yaliyopo katika Mkoa wa Morogoro na ni moja kati ya sehemu ambazo zimeathiriwa na mvua kwa wingi huku kilio kikubwa kwa wananchi ni kuboresha barabara.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments