WANANCHI KATA YA KINDAI MANISPAA SINGIDA WAMSHUKURU RAIS Dkt. SAMIA.

WANANCHI wa Kata ya KINDAI Manispaa ya Singida wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kutoa Fedha nyingi za kuboresha miundombinu mbalimbali ya maendeleo katika Kata hiyo ya KINDAI.

Diwani wa Kata hiyo OMARY KINYETO alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa KINDAI akiwa katika Ziara yake ya kuzungumza na Wananchi wa Kata hiyo akielezea utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kata ya KINDAI.

Alisema Fedha hizo zilizotolewa na Rais SAMIA zimetumika katika sekta ya Elimu, Afya na Barabara ili ziweze kutatua changamoto ya upungufu wa Madarasa yaliyoisaidia kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasani, Vifaa Tiba na miundombinu katika sekta ya Afya na Ujenzi wa Barabara.

KINYETO alisema kupitia Miradi hiyo ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali wananchi wa Kata ya KINDAI wanapata huduma kwa urahisi na kuacha kutembea umbali mrefu kufuata hudumu za Jamii.

Hata hivyo aliomba Serikali kuongeza madarasa kwa ajili ya watoto wa darasa la Awali (chekechea) ambao wamekuwa wengi na kusababisha msongamano wa watoto hao katika Madarasa mawili (2) ambayo yapo kwa sasa katika Shule ya Msingi Kindai.

Aidha KINYETO aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na kuhakikisha CCM inashinda katika ngazi zote za uongozi.
                          
Pia aliwataka wananchi hao kuchukua Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa wale ambao wanasifa za kuwa viongozi Bora ambao wanaweza kutatua changamoto za wananchi.

Alisema wananchi wahakikishe wanachagua viongozi ambao wanauwezo wa kutatua changamoto zao na sio kuchagua Viongozi ambao hawatatui changamoto za wananchi.

Aidha KINYETO aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mabalozi ili kurahisisha utendaji kazi wa mabalozi wa Kata hiyo na utekelezaji wa Ilani ya CCM.

KINYETO alisema Serekali inapotaka kufanya jambo lolote huenda kwa Wenyeviti na Mabalozi wa Serikali za Mitaa ili kujua namna ya kutekeleza Miradi ya maendeleo.









TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments