WANANCHI TOENI TAARIFA ZA WAHALIFU KWA MAMLAKA HUSIKA .

DIWANI wa Kata ya Kindai Manisapaa ya Singida OMARY KINYETO amewataka wananchi kutoa taarifa za Uhalifu na Wahalifu ili kukomesha vitendo vya Uhalifu katika Kata hiyo ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya wananchi.

KINYETO alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Singida Monangi katika Kata hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya Kata hiyo ikiwemo Maendeleo na Usalama.

Alisema wahalifu wengi wanajulika kwani wapo katika nyumba zetu, hivyo ni vizuri kuwataja ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria
                       
KINYETO aliongeza kuwa kuna baadhi ya wahalifu wamekuwa wakihatarisha maisha ya watu, hasa wakati wa kuwapora mali zao kwa kuwajeruhi vibaya na wakati mwingine kukatisha maisha yao kwa kuwapiga.

Alisema sababu kubwa ya kuwepo kwa vitendo vya Uhalifu ni baadhi ya wananchi kuuza Pombe kinyume na sheria na taratibu za nchi, ambapo wamekuwa wakiuza pombe mpaka saa Nane (8) za usiku.
                         
Alisema kutokana na kufanya biashara hizo za pombe mpaka saa Nane za usiku imekuwa sababu kubwa ya kuongezeka kwa vitendo vya Uhalifu katika Kata hiyo ya Kindai.

Hata hivyo wale wote wanaouza pombe wametakiwa kuacha kuuza pombe ifikapo saa Nne usiku na sio saa Nane usiku, ili kuzuia vitendo hivyo vya uhalifu.
                            

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Singida Monangi FATUMA HASSAN aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuzuia vitendo vya Uhalifu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi kuanzisha Vikundi vya Ulinzi shirikishi ambavyo vitasaidia kufanya ulizi nyakati za usiku.

                                 

Na Mwandishi Wetu Singida Rafuru Kinala.
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments