WATUHUMIWA 235 WAKAMATWA SINGIDA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limewakamata watuhumiwa 235 wa Makosa mbalimbali ya Jinai na vielelezo vinavyowaunganisha watuhumiwa na Makosa yao kwa kipindi cha Mwezi Febuari hadi April mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida AMON  KAKWALE amesema hayo wakati akizungumza na Waadishi wa Habari akitoa Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa huo kwa kipindi cha Mwezi Februari hadi April mwaka huu.

                             
KAKWALE alisema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia, Doria na Misako mbalimbali zilizofanywa na Jeshi Polisi kwa kushirikiana na wananchi kwa lengo la  kuzuia uhalifu na kuendelea kuweka Usalama wa Raia na Mali zao.

Alisema kati ya watuhumiwa hao, 135 walikamatwa na Madawa ya kulevya aina Bangi yenye uzito wa Kilogramu 17.2.

                           
KAKWALE pia alisema watuhumiwa wengine 46 walikamatwa na dawa za kulevya aina Mirungi, zenye uzito wa Kilogramu 92 na kuwa upepelezi unaendelea ili kuwafikisha mahakama taratibu zote zitakapokamilika.

                          
Aliongeza kuwa kuna baadhi ya Kesi Upelelezi wake bado unaendelea na zingine watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani na Kesi zao bado zinaendelea kusikilizwa, huku watuhumiwa wengine wakihukumiwa vifungo mbalimbali kutokana na makosa yao.
Aidha aliwashukuru Wananchi wa Mkoa wa Singida kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi hali iliyosababisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao 235.

Hata hivyo Kamanda KAKWALE aliwataka wananchi kuendelea kutoa tarifa mbalimbali za wahalifu ili Jeshi la Polisi liweze kudhibiti vitendo hivyo vya uhalifu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments