ZAIDI YA WANAFUNZI 50 WA SHIRIKA LA HAND IN HAND WAPATIWA MAFUNZO KIJIJI CHA NYUKI

                                   

Zaidi ya Wanafuzi 50 kutoka Shirika lisilo la kiserikali la HAND IN HAND kutoka mkoani Manyara wametembelea Kijiji cha Nyuki Kisaki Singida kujifunza masuala mbalimbali ya Ufugaji Nyuki kibiashara yanayofanyika kijiji hapo.


Akizungumzia na wanafunzi hao Meneja wa Kijiji cha Nyuki ELBARIKI KIEMI alisema Kijiji cha Nyuki kimekuwa kikitoa Mafunzo na Elimu kupitia Shule iliyopo kijijini hapo kwa wananchi wa Mikoa mbalimbali ili kuongeza Wafugaji wa Nyuki nchini wanaofuga Nyuki kibiashara.

ELBARIKI alisema kufuga Nyuki kibiashara kunamfanya Mfugaji wa Nyuki kuvuna mazao mengi yatokanayo na mdudu Nyuki tofauti na watu wengi waliozoea kuvuna Asali na Nta tu.
                         

Alisema kupitia Ufugaji wa Nyuki kibiashara mtu atavuna mazao yatokanayo na Nyuki kama vile, Maziwa ya Nyuki, Vumbi la Singida, Sumu ya Nyuki, Gundi ya Nyuki na mazoea Mama yatokanayo na Nyuki Asali na Nta.

Aidha ELBARIKI alitoa wito kwa wananchi wanaotaka kujihusisha na ufugaji wa Nyuki kibiashara waeende Kijiji cha Nyuki kupata mafunzo yatakayowasaidia kuzalisha mazao mengi yatokanayo na Nyuki na waweze kuongeza vipato vya familia zao na Taifa kwa ujumla.

ELBARIKI aliongeza kuwa kupitia Ufugaji Nyuki, Kijiji cha Nyuki kimekuwa na mchango mkubwa katika kutunza Mazingara kwani Nyuki wanahitaji mazingira mazuri yenye Miti na Vichaka ili waweze kufanya uzalishaji wao kwa urahisi.
                            
Hivyo aliwataka wanafunzi hao kuwa watunzaji wazuri wa Mazingira katika maeneo yao ili ufugaji wa Nyuki uwe na tija kwani ufugaji huo hutegemea mazingira ya Miti na Vichaka kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo alisema Kijiji cha Nyuki kinafanya Tafiti mbalimbali zinazomhusu Nyuki katika kuzalisha mazao mbalimbali yatokanayo na mdudu huyo Nyuki ili kufanya uzalishaji wa mazao ya Nyuki unaongezeka nchini.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano na Biashara wa HAND IN HAND Tawi la Mkoa wa Manyara PASCALINE ISRAEL  aliishukuru Kampuni ya Kijiji cha Nyuki kwa kuwapa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kufuga Nyuki kibiashara.

PASCALINE alisema kuwa watakuwa Mabalozi waziri wa kwenda kuisambaza Elimu hiyo kwa wananchi wengine ili iweze kuwafikia watanzania wengi.

Hata hivyo wanafunzi hao wametembelea Mazingira ya Kijiji cha Nyuki ikiwemo Mashamba ya Mizinga, Maporomoko ya Maji, Kiwanda cha Asali, na vivutio mbalimbali vya Utali vilivyopo Kijiji cha Nyuki Kisaki Singida.





                              



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments