BILIONI 30 KUIMARISHA HUDUMA ZA WATOTO WACHANGA KATIKA HOSPITALI 100 NCHINI

 Serikali kupitia Wizara ya Afya imepanga kutumia shilingi bilioni 30 kuimarisha huduma za watoto wachanga kwenye hospitali 100 nchini kwa kujenga wodi maalum (NCU) za Watoto wachanga, Watoto njiti na ununuzi na usambazaji wa vifaa tiba ikiwemo mashine za kuwasaidia Watoto wachanga njiti kupumua.

Hayo yamebainisha na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Bungeni jijini Dodoma Juni 03,2024 wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu katika bunge la 12, mkutano wa 15 na kikao cha 39

Dkt. Mollel amesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali ilipeleka vifaa vya kusaidia Watoto njiti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya 241 vyenye jumla ya thamani ya bilioni 2.6 hadi kufikia machi 2024.

Wakati huo huo Dkt. Mollel ameweka msisitizo kuwa, Serikali kupitia Sera ya Afya ya Mwaka 2007 imeweka utaratibu wa Wagonjwa wote wa dharura kupatiwa huduma za Afya za dharura kwanza pasipo kikwazo cha kulipia huduma hadi atakapo tatuliwa changamoto za kiafya zinazo mkabili.

“Natoa wito kwa waganga wakuu wa vituo vyote kuhakikisha wagonjwa wa dharula wanapata huduma wanazostahili kwanza ili kuokoa Maisha yao na taratibu nyingine zifuate baada ya kuwa wamehudumiwa”, ameelekeza Dkt. Mollel.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments