Dirisha la usajili Bara lafunguliwa Jana

DAR ES SALAAM – DIRISHA la usajili kwa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Ligi ya Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa mwaka 2024/25 litafunguliwa leo na kufungwa Agosti 15, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kupitia kwa Ofisa Habari wake, Clifford Ndimbo jana imesema klabu zinatakiwa kuanza kufanya usajili na uhamisho wa wachezaji wao kwa msimu wa mwaka 2024/25.

“Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili na klabu zote zinaombwa kuzingatia muda huo wa usajili na uhamisho na tunaziomba kuwasiliana na idara ya mashindano ya TFF kama kuna changamoto zozote,” ilisomeka taarifa hiyo ya TFF.

Aidha, taarifa hiyo ilisema usajili na uhamisho wa wachezaji kwa dirisha dogo utakuwa Desemba 16, 2024 na kufungwa Januari 15, 2025.

Katika hatua nyingine TFF imesema maombi ya klabu kwa njia ya mtandao kwa klabu zitakazoshiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika kwa msimu wa mwaka 2024/25 Juni 15, mwaka huu.

Klabu itakayotimiza masharti ya leseni hizo ndio itakayoruhusiwa kushiriki kwenye mashindano hayo, hivyo TFF inazikumbusha klabu zote kufanya maombi kwa wakati kwani hakutakuwa na muda wa ziada baada ya tarehe ya mwisho.

Taarifa hiyo iliongeza klabu itakayokuwa inadaiwa na kocha, mchezaji au mfanyakazi inatakiwa kulipa deni hilo na kinyume chake haitaruhusiwa kushiriki mashindano ya Caf.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments