RAIS SAMIA NI KIELELEZO CHA USTAHIMILIVU NA MAENDELEO TANZANIA,ASEMA MLATA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Singida, Martha Mlata amefurahishwa na mafanikio lukiki ambayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewaletea wananchi.

Akizungumza na wananchi na wanachama wa chama  hicho, Martha amesema Rais Samia ameleta maendeleo makubwa ambayo hayakuwahi kutokea tangu kupatikana uhuru wa nchi hii.

Martha ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kidarafa, Kata ya Mwanga wilayani Mkalama mkoani Singida.

Aidha Martha amewaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia kwasababu amejipambanua kumjali kila mtanzania popote alipo huku akiwaasa  kuendelea kuwa watulivu kwa sababu  serikali ya CCM inaendelea kutekeleza ilani kwa kishindo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments