MAZINGIRA MAZURI YAMEWEKWA NA RAIS SAMIA,ASEMA MARTHA MLATA

                                     

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida MARTHA MLATA amesema Serikali itaendelea kudumisha Amani, Utulivu na Muungano wa Tanzania ili Wananchi waendelee kufanya shughuli mbalimbali kwa utulivu za kujiletea maendeleo kwa  Taifa kwa ujumla.


MLATA alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna faida yoyote, na kwamba wanasiasa hao sio wakiwasikiliza wala kufuata maneno yao kwani hawalitakii mema Taifa letu.

Aidha MLATA aliendelea kusema Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya Barabara ili wananchi waweze kusafirisha mazao yao kwenda sokoni kwa urahisi na kupata huduma zingine ambazo zinahitaji miundombinu mizuri ya barabara.

                
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida MARTHA MLATA aliwataka wananchi kuacha kuwafuata wanasiasa wanaohamasisha Wananchi kuacha kujitokeza kupiga kura wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

MLATA alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa hadhara katika Kata Msange, kijiji cha Mangida Halmashauri ya Singida Vijijini, kuwahamasisha wananchi hao kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

                
Alisema kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipita pita katika maeneo mbalimbali kuwataka wananchi kuacha kupiga Kura katika chaguzi zijazo, wakati ni haki yao ya kikatiba ya kuchagua Viongozi.

MLATA aliwataka wananchi wasidanganyike kwa maeneo ya wanasiasa hao na badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga Kura katika maeneo yao na wachague viongozi ambao watasaidia kutatua changamoto zao.
                
Kwa upande wake MNNEC wa Mkoa wa Singida YOHANA MSITA aliwataka wananchi waendelee kukiamini na kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi CCM  katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

MSITA aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi huo wa serikali za Mitaa na kuwachagua viongozi watakaosimamishwa na CCM kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
               
Alisema kupitia CCM wananchi wameendelea kupata maendeleo kwani serikali chini ya CCM inatekeleza miradi mingi ya maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Aidha aliwataka wananchi kuacha kuwafuata wanasiasa wanaochochea chuki za ubaguzi wa Ukabila, Udini na Ukanda kwa maslahi yao binafsi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments