RC DENDEGO AENDELEA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI MKOANI SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ameendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi ikiwa ni mwendelezo wa kampeni aliyoizindua hivi karibuni.

Dendego ameendesha kampeni hiyo, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kidarafa Kata ya Mwanga wilayani Mkalama mkoani Singida.

Amesema amedhamiria kwa dhati kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero kwa lengo la kuwaacha salama wakiendelea na shughuli za uzalishaji mali unaoendelea kuwepo kutokana na utulivu aliouweka Rais Dk. Samia Suluhu nchini.

Dendego katika kampeni hiyo  ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Martha Mlata, Katibu wa Chama hicho, Lucy Shee, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa mkoa huo, Elphas Lwanji Mkuu wa Wilaya hiyo, Moses Machali na viongozi wengine.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments