WADAU SEKTA YA UJENZI WAJENGEWA U UWEZO KUKABILIANA NA MIGOGORO KWA NJIA RAFIKI

Serikali kupitia Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) imejipanga kupunguza migogoro katika sekta ya ujenzi kwa kuwajengea uwezo wadau mbalimbali jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa suluhishi kwa kutumia njia rafiki inayotoa fursa kwa pande mbili kuelewana bila kwenda Mahakamani.


Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa sekta ya ujenzi kuhusu namna bora ya utatuzi wa migogoro yalioratibiwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Mkadiriaji Majenzi wa NCC, Bw. Elias Kissamo, amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kuwa na elimu ya namna ya bora kufanya utatuzi wa migogoro nje ya mahakama.

Bw. Kissamo amesema Baraza la Taifa la Ujenzi limeundwa kwa ajili kuangalia maendeleo ya ujenzi nchini ikiwemo kuwa na njia sahihi za kusimamia katika usuluhishi migogoro.

“Baraza linasimamia usuluhisi na sio msuluhishi kwani linachagua wasuluhishi ambao wapo kwenye mpangilio wanaosaidia katika kusuluhisha’amesema Bw. Kissamo.

Rais wa Chama Cha Mawakili Afrika Mashariki, Jaji Mstaafu wa Mahakama kuu ya Tanzania Dkt. Fauz Twaib, amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa migogoro imeonekana kuwe na haja ya kuwa na mfumo mbadala mbali na mahakama kwa ajili ya kutatua migogoro.

“Kuna mambo mengi ambayo unaweza kuyaepuka kwa kutumia mfumo mbadala mmoja wapo ni kujaribu kupunguza muda ambao utatumika kutatua migogoro kwani unapokwenda
mahakani utachukua muda mrefu zaidi, pia mahakama ina utaratibu lazima uufate ili uweze kutatu
migogoro” amesema Dkt. Twaib.

Mshiriki wa mafunzo hayo Wakili wa Serikali Bi. Rehema Mtulya, amesema kuwa mafunzo hayo yatamsaidia katika
uendeshaji wa mashauri ya usuluhishi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.

Bi. Mtulya ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuhudhuria mafunzo hayo kwani yanakwenda kupunguza migogoro katika sekta ya ujenzi nchini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments