Watumishi wa Afya nchini wametakiwa kwenda kufanya kazi katika Halmashauri za pembezoni mwa nchi ili kupunguza uhaba wa wataalamu hao unaokadiriwa kuwa ni zaidi ya asilimia 50.
Upungufu huo unaovikabili vituo vya Afya, Zahanati na baadhi ya Hospitali za Halmashauri umechangia kudhoofisha hali ya utoaji wa hudumaza Afya.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Julai 29, 2024 wakati wa Kongamano la kumbukizi la Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa lililoandaliwa na taasisi ya Mkapa Foundation lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaa.
“Niwatoe hofu watumishi wa Afya kutoogopa kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni mwa nchi kwa kuwa huduma zote muhimu za kijamii zinapatikana ikiwemo umeme, barabara, maji pamoja na shule.” Amesema Waziri Ummy
Amesema, leo mkutano huo utajadili masuala ya rasilimali watu kwenye Sekta ya Afya ambao ni uzalishaji wa wataalamu wa Afya ndani ya nchi, ubora wa watumishi wa Afya kwa kuhakikisha watumishi wanasalia kwenye maeneo waliyopangiwa kuhudumia wananchi.
Waziri Ummy amesema Hayati Rais Benjamini Mkapa alikua ni muumini na kinara waliofanya kazi kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za Afya ikiwemo Sheria ya Bima ya Afya ya NHIF aliyoiasisi Mwaka 2,000.
Waziri Ummy amesema, hivi sasa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) umekua ndio chanzo kikuu cha mapato yanayotokana na huduma zinazotolewa kupitia mfuko huo.
Kongamano hilo linakutanisha wadau mbalimbali katika Sekta ya Afya ambapo watajadili masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya ambapo linatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Julai 30, 2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
“Tunategemea kupata maoni na ushauri wa wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya ikiwemo Sekta binafsi katika kutengeneza mkakati wa Sita wa Taifa wa Sekta ya Afya Mwaka 2026/2031 ambao inaendana na kukamilisha kwa dira ya Taifa ya Mwaka 2050.” Amesema Waziri Ummy
Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya Benjamin Mkapa, Rahel Sheiza, amesema dhamira kubwa ya kuitisha kongamano hilo ni kuona haja ya kutatua rasilimali watu kwa njia mtambuka.
“Taasisi yetu kwa zaidi ya miaka 18, imejikita kuongeza nguvu kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa watumishi wa afya sio tu kwa namba, bali sifa na utendaji,pia kuhakikisha mifumo ya rasilimali fedha katika sekta ya afya hatuitegemei serikali tunatafuta vyanzo vingine vya kiubunifu,” amesema.
Amesema taasisi yao imeweza kuchangia watumishi 5200 ambao wapo katika maeneo ambayo yanachangamoto ya watumishi, lakini wameshirikiana na wadau mbalimbali kuweza kupeleka watumishi hao katika ngazi za vituo.
“Pia tumepeleka watumishi wa afya ngazi ya jamii, tumejenga nyumba 480 kwa sababu changamoto moja wapo ni uhaba wa nyumba, pia tumeweza kutoa mafunzo, kushirikiana na taasisi mbalimbali tumeweza kuongeza rasimali fedha katika kuhakikisha tuna rasilimali afya yenye tija na uwezo wa kufanya kazi,” amesema.
Waziri wa Afya , Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa Kongamano la Kumbukizi la Rais Mstaafu Hayati Benjamini William Mkapa lililofanyika leo Julai 29,2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya Benjamin Mkapa, Rahel Sheiza,akizungumza wakati wa Kongamano la Kumbukizi la Rais Mstaafu Hayati Benjamini William Mkapa lililofanyika leo Julai 29,2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

0 Comments