BARRICK NORTH MARA YAADHIMISHA SIKU YA INI DUNIANI KWA BONANZA LA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE

 

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko (mwenye kofia katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mchezo wa pete kwenye uwanja wa mgodi huo
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barick North Mara, Apolinary Lyambiko (wa sita kushoto mbele) na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo wakati wa uzinduzi wa bonanza la michezo mgodini hapo
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Baarick North Mara, Apolinary Lyambiko akifungua mchezo wa mpira wa kikapu mgodini hapo
Wafanyakazi wa mgodi wa North Mara wakicheza mpira wa kikapu mgodini hapo
Wafanyakazi wa mgodi wa North Mara wakicheza mpira wa pete mgodini hapo

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara umehitimisha mwezi wa kampeni dhidi ya maradhi ya Homa ya Ini (Hepatitis B) kwa wafanyakazi wake kushiriki bonanza la michezo mbalimbali.

Kupitia kampeni hiyo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani inayoadhimishwa Julai 28, wafanyakazi wa mgodi huo walijengewa uelewa juu ya maradhi hayo na namna ya kujikinga na maambukizi yake.

Akizungumza kabla ya kuzindua bonanza la michezo hiyo katika viwanja vya mgodi wa North Mara , Meneja Mkuu (GM) wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko, aliwahimiza wafanyakazi wote kupata huduma za vipimo na chanjo ya Homa ya Ini zinazotolewa mgodini hapo.

Kuhusu michezo, GM Lyambiko, aliwataka washiriki wote kushindana kwa amani, upendo na furaha ili kujiimarisha kiukakamavu na kujenga afya ya akili na mwili.

Meneja wa Afya na Usalama wa Mgodi wa North Mara, Dkt Nicholas Mboya alisema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa programu maalumu iliyoanzishwa na mgodi huo kwa ajili ya wafanyakazi wake

Kwa upande wake Dkt. Abdulnur Maupa kutoka mgodi huo alisema chanjo dhidi ya ugonjwa huo inahusisha sindano tatu na inapatikana kwenye kliniki mbili zilizopo ndani ya mgodi huo.
Pia, Dkt Maupa alisema ugonjwa wa Homa ya Ini husababishwa na unywaji wa pombe uliokithiri, matumizi ya dawa yasiyo sahihi, kuchangia vifaa vyenye ncha kali na ngono uzembe (isiyo salama).

Michezo ambayo wafanyakazi walishiriki ni pamoja na mpira wa pete, kikapu, miguu, kukimbia, kufukuza kuku na kukimbia kwenye magunia.

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unamilikiwa kwa ubia kati ya kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Gold Corporation na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya taifa ya Twiga Minerals.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments