WADAU mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, baadhi ya wabunge na Umoja wa Mashirika yasiyo ya Serikali (CAMAC) wamekutana na kujadili sheria na haki zinazogusa Afya ya Uzazi.
Katika mkutano huo iliongelewa kuwa kuna umuhimu wa kuwasaidia wasichana na wanawake waliopata mimba kutokana na ukatili kama kubakwa,maharimu na shambulio la ngono.Wahanga hawa kusaidiwa ili kuepusha utoaji wa mimba usio salama ambao unachangia kwa asilimia 10% wa vifo vitokanavyo na uzazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Chama cha Uzazi na Malezi bora (UMATI) Suzanne akizungumza na Wanahabari Leo Julai 30,2024 wakati wa Mkutano huo amesema mwaka 2007 sheria iliruhusu kuwepo kwa Haki ya Mtu kutoa Mimba pale inapobainika kuwa ujauzito huo unaweza kumsababishia matatizo .
Amesema Chama hicho kipo Kwa ajili ya kuwawakilisha Wanawake wengine na kuwapa mwanga atika swala zima la kuhusu haki zao kiafya.
Mtoa huduma kwa Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Muhimbili profesa Barnabas Pembe ameeleza kuwa amekuwa mbobezi wa kutoa huduma za kitabibu kwa Wanawake kwa takribani miaka 32.
Amesema huduma za afya ya uzazi nchini zimekuwa zikiongezeka na kuboreshwa siku hadi siku.
Pembe amesema Teknolojia inakuwa kwa Haraka zaidi huduma kuendelea kuwa bora zaidi pamoja na kuongezeka kwa vituo vinavyotoa vituo huduma kwa maswala ya Uzazi.
Pia amesema Utoaji Mimba kwa Tanzania inaruhusiwa lakini katika baadhi ya maeneo ikibainika uhai wa Mama upo hatarini.
Pia amesema Majadiliano kama hayo Yana Afya ili yaweze kusaidia Jamii ambapo ipo ndani ya Tanzania na kuhakikisha haileti Matatizo kwa jamii kutokana na watu kuwa wa wazi na huru kutoa Mawazo yao kwa kutumia mila na desturi na Kidini .
Nae Wakili wa Kujitegemea Baraka Thomas amesema kwa Mujibu wa sheria kanuni ya adhabu sura Namba 16 inaeleza utoaji wa mimba ambao haukufata sheria ni kosa la jinai ambalo linapeleka mtu alihusika kumtoa mimba Mama huyo kushtakiwa na atakutwa na Hatia kifungo cha Miaka 14 au akiwa Mwanamke Mwenyewe amesababisha atakutwa na hatia kifungo Miaka 07.
Amesema sheria hiyo inaruhusu mimba kutolewa endapo tu maisha ya mama yako hatarini lengo likiwa ni kulinda uhai.
Pia ameongeza kuwa wadau wamejadiliana kuona namna ya kudhibiti utoaji mimba usio salama.
0 Comments