Diwani Urio ashinda unaibu Meya Kinondoni

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, wamemchagua Michael Urio (Diwani wa Kata ya Kunduchi ), kuwa Naibu Meya Mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Michael Urio ameshinda uchaguzi wa kiti cha unaibu Meya kwa kura 16 kati ya 26 za wabunge na madiwani wa kinondoni kwenye uchaguzi uliofanyika LEO.

Uchaguzi huo umefanyika ikiwa ni baada ya kumalizika kwa kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Naibu Meya aliyekuwa madarakani ambaye ni Joseph Rwegasira.

Uchaguzi huo wa ndani ya chama cha mapinduzi ulihusisha wagombea wawili ambao ni Joseph Rwegasira aliyekuwa akitetea kiti chake na Michaeli Urio (Diwani wa Kunduchi)

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Urio alisema , “Ninawashukuru sana waheshimiwa madiwani kwa kuonyesha imani kubwa kwangu, naomba niwahakikishie kwa kushirikiana na Mstahiki meya tutahakikisha tunafanyakazi kwa pamoja ili kuwaletea maendeleo wananchi wetu ndani ya Manispaa yetu ya kinondoni.”

Uchaguzi huo ulisimamiwa na Meya wa Kinondoni Mnyonge Songoro, ambae alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi songoro.

Akizungumza kwa niaba ya chama cha mapinduzi Mwendez wa CCM wilaya ya Kinondoni Lilian Lwebangila alisema chama cha mapinduzi ni wako,mavu katika chaguzi na aliwaasa Naibu Meya aliyemaliza muda na huyu alieshinda kushirikiana katika kuijenga Kinondoni

Makundi hayakosi ndani ya chaguzi lakini baada ya kumalizika kwa uchaguzi sisi woote ni wamoja alimaliza na kumponeza Urio kwa kuteuliwa kuwa Naibu Meya Kinondoni.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments