Hamisa: Nilimshauri Aziz Ki asiondoke

DAR ES SALAAM; Baada ya Hamisa Mobetto kuhusishwa na nyota wa Yanga, Azizi Ki, mwanamitindo huyo amevunja ukimya juu ya sakata hilo.

Amesema picha na video zinazoendelea katika mitandao ya kijamii kati yake na Ki ni kwa sababu ni rafiki yake wa karibu.

 

“Nilimwambia Azizi Ki asiondoke, ndio mana niliandika maneno kama angeondoka ingekuwaje? Na kama Azizi Ki angeondoka ningepanda ndege kumfata popote alipo, “amesema Hamisa na kuongeza kuwa Ki ni mchezaji mzuri.

Soma:Hersi: Aziz Ki anabaki

“Binafsi sikufatwa na mtu yoyote kumshawishi Azizi Ki kubaki, bali nilimsahuri na yeye ameamua mwenyewe ukizingatia ni mchezaji mzuri anastahili kuendelea kucheza katika timu hiyo.

Pia mwanamitindo huyo amesema amefungua duka Tandika jijini Dar es Salaam, liitwalo Mobettostyles Tandika Plaza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments