Maandalizi NBC Dodoma Marathon Yakamilika, RC Dodoma Awataka Wananchi Kuchangamkia Fursa

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi Rosemary Senyamule amethibitisha kukamilika kwa maadalizi ya msimu wa tano mbio za NBC Dodoma Marathon huku akionyesha kuridhishwa na ubora wa mbio hizo sambamba na mchango wake katika kuchochea kasi ya Uchumi wa mkoa huo kupitia sekta za biashara, michezo na utalii.


Mbio zinatarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma zikiwa na lengo la kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama na mtoto. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza washiriki zaidi ya 8,000 waliothibitisha kushiriki mbio hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo RC Senyamule pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa maandalizi hayo mazuri alisema ujio wa mbio hizo mkoani humo kwa miaka mitano sasa umekuwa ukiambatana na fursa mbalimbali ikiwemo ongezeko la mzuguko wa fedha unaotokana na ongezeko la mahitaji ya chakula, vinywaji,mavazi na malazi kutona na idadi kubwa ya watu wanaotoka mikoa mbalimbali ili kushiriki mbio hizo jijini humo.

“Kukamilika kwa maadalizi ya mbio hizo tena katika viwango vya kimataifa kunatoa taswira sahihi ya hadhi ya mbio hizo na jiji la Dodoma kama makao makuu ya nchi. Nitoe wito kwa wananchi wa jiji la Dodoma hususani wafanyabiashara kuchangamkia fursa mbalimbali zitokanazo na ongezeko hili la watu ambao nje ya washiriki hao 8,000 waliothibitisha kushiriki pia wapo wengine zaidi walioambatana nao.’’ Alisema.

Aidha, Bi Senyamule aliowamba washiriki wa mbio hizo kutumia fursa hiyo pia kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyomo mkoani humo ukiwemo utalii wa majengo ya serikali kama vile Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Mji wa serikali sambamba na utalii wa utamaduni ikiwemo ngoma za asili za wenyeji wa mkoa huo ambao ni kabila la Wagogo huku pia wakipata wasaa wa kujionea kilimo cha zao la zabibu ambalo kwa Afrika Mashariki linalimwa mkoa huo pekee.

“Zaidi nitoe wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kandokando ya Barabara ili kushangilia na kuwapa nguvu washiriki wa mbio hizo watakaotumia baadhi ya barabara hapa mjini. Kwa wale ambao hawatakuwa na ulazima wa kutumia magari yao ni vema wasiingie nayo barabarani ili kupunguza msongamano wa vyombo hivyo barabarani ili kuepuka ajali na usumbufu kwa washiriki wa mbio hizi,’’ aliongeza.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, ambayo ndio inaratibu mbio hizo Bw Godwin Semunyu alisema maandalizi yote yamekamilika na tayari washiriki mbalimbali wa mbio zinazohusisha umbali wa km 5, km 10, km 21 na km 42 wanaendelea kuingia jijini humo ili kushiriki mbio hizo.

“Ili kuongeza mchango wa mbio hizi kiuchumi na burudani zaidi tumebuni matukio kadhaa likwemo tamasha la kuonja mvinyo yaani ‘Wine Testing Festival’ litakalofanyika Julai 27 hapa Dodoma na zaidi tumeandaa matukio mengine ya burudani za vichekesho na tafrija mbalimbali lengo likiwa ni kuongeza burudani wa washiriki wa mbio hizi hususani wageni huku pia tukilenga kuchochea mzunguko wa fedha ili kuwanufaisha zaidi wenyeji wa jiji hili,’’ alisema Semunyu huku akiwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo wadhamini wa mbio hizo kufanikisha matukio hayo.

Akuizungumza kwa niaba ya wadau hao, Mkuu wa Kanda ya Kati wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Bw Joseph Sayi alisema kampuni hiyo ikiwa kama mdau mkuu wa mawasiliano kwenye mbio hizo imejipanga kutoa huduma ya mawasiliano ya internet bure kwa washiriki wote wa mbio hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Rosemary Senyamule  (wa pili kulia) akipokea sweta maalum la mbio za NBC Dodoma Marathon kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bi Tasiana Massimba (Kulia) ikiwa ni ishara ya kumkaribisha rasmi mkuu wa mkoa huyo kwenye mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Mbio hizo zinalenga kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na  kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga  ili kuboresha afya ya mama na mtoto makabiziano hayo yamefanyika  makao makuu ya benki hiyo jijini Dodoma leo. Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Joyce Fisoo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Rosemary Senyamule  (kulia) akitapata maelezo kuhusu alama mbalimbali ziliwekwa kwenye sweta maalum la mbio za NBC Dodoma Marathon kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu (wa pili kushoto) baada ya kukabidhiwa sweta hilo ikiwa ni ishara ya kumkaribisha rasmi mkuu wa mkoa huyo kwenye mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Mbio hizo zinalenga kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na  kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga  ili kuboresha afya ya mama na mtoto makabiziano hayo yamefanyika  makao makuu ya benki hiyo jijini Dodoma leo. Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Joyce Fisoo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Rosemary Senyamule  (katikati) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya fulana maalum  za mbio za NBC Dodoma Marathon mwaka 2024 mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bi Tasiana Massimba (Kulia) ikiwa ni ishara ya kumkaribisha rasmi mkuu wa mkoa huyo kwenye mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Mbio hizo zinalenga kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na  kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga  ili kuboresha afya ya mama na mtoto makabiziano hayo yamefanyika  makao makuu ya benki hiyo jijini Dodoma leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo RC Senyamule (pichani) pamoja na kuipongeza benki ya NBC  kwa maandalizi hayo mazuri alisema ujio wa mbio hizo mkoani humo kwa miaka mitano sasa umekuwa ukiambatana na fursa mbalimbali ikiwemo ongezeko la mzunguko wa fedha unaotokana na ongezeko la mahitaji ya chakula, vinywaji,mavazi na malazi kutona na idadi kubwa ya watu wanaotoka mikoa mbalimbali ili kushiriki mbio hizo jijini humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon Bi Tasiana Massimba (Pichani) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28, mwaka huu jijini Dodoma.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, ambayo ndio inaratibu mbio hizo Bw Godwin Semunyu (pichani) alisema maandalizi yote yamekamilika na tayari washiriki mbalimbali wa mbio zinazohusisha umbali wa km 5, km 10,km  21 na km 42 wanaendelea kuingia jijini humo ili kushiriki mbio hizo.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkuu wa Kanda ya Kati wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Bw Joseph Sayi (pichani) alisema kampuni hiyo ikiwa kama mdau mkuu wa mawasiliano kwenye mbio hizo imejipanga kutoa huduma ya mawasiliano ya internet bure kwa washiriki wote wa mbio hizo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon wakifutilia mkutano huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments