TETESI za usajili zinasema Manchester City inafikiria uhamisho wa winga wa Crystal Palace, Eberechi Eze, huku nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa na kipengele cha kuachiwa cha pauni milioni 60 pamoja na nyongeza. (Mirror)
Klabu ya Saudi Arabia, Al-Ittihad inamtaka kiungo wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, hatua ilisababisha Manchester City kufikiria dili la kumsajili Eze. (Guardian)
Eze mwenye kipaji amekuwa katikati ya harakai za vilabu mbalimbali vikionyesha nia ya kumsajili.
Kiwango chake kizuri msimu uliopita akiwa na Crystal Palace kimemfanya kuwa lengo muhimu kwa timu zinazotaka kuboresha vikosi vyao. Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England na vingine vya Ulaya vinavyohusishwa na nia ya kumsajili nyota huyu mdogo.
SOMA: Tetesi za usajili Ulaya
Majadiliano kuhusu usajili wake yamekuwa magumu kutokana na msimamo wa Crystal Palace wa kutaka kumbakiza Eze.
Uongozi wa klabu hiyo unaripotiwa kuwa unataka tu kuzingatia ofa zitakazokubaliana na thamani ya mchezaji huyo, ikionyesha azma yao ya kumbakiza mchezaji muhimu.
Licha ya nia kubwa kutoka kwa vilabu kama Liverpool na Tottenham, bei inayotakiwa na Palace imekuwa kikwazo. Majadiliano yanaendelea, huku pande zote mbili zikijaribu kupata muafaka.
Hali hiyo imeongeza minong’ono katika jamii ya soka, huku mashabiki na wataalamu wakihusisha uwezekano wa mchezaji huyo kuhamia klabu nyingine.
Kwa sasa, Eze anaendelea na kuwepo Crystal Palace, huku dunia ya soka ikisubiri kuona kama atabaki Selhurst Park au ataanza maisha mapya ya soka katika klabu nyingine.
Manchester City ina nia kumsajili golikipa wa Paris St-Germain na Italia Gianluigi Donnarumma, 25, wakati ikipanga mbadala wa golikipa wa Brazil Ederson, 30, ambaye huenda akahamia Al-Ittihad. (Sky Sports Italy)
Ederson ataigharimu Al-Ittihad angalau pauni milioni 40, lakini Manchester City inakusudia kumruhusu kuondoka iwapo thamani yake itafikiwa. (ESPN)
Paris Saint-Germain inahitaji huduma ya winga wa Manchester United Jadon Sancho, 24, na fowadi huyo anaonekana kuwa tayari kujiunga na mabingwa hao wa Ufaransa. (Foot Mercato – in French
Pia PSG ina nia kumsajili kiungo wa Manchester United na Ureno Bruno Fernandes, 29. (L’Equipe – in French)
Everton inajiandaa kumpa ofa iliyoboreshwa beki wake Jarrad Branthwaite, 22, ikiwa ni katika juhudi za kumshawishi kuikataa Manchester United. (Fabrizio Romano)
Aston Villa inalenga kumsajili fowadi wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 24, baada ya kukubali kumuuza winga wa kifaransa Moussa Diaby, 25, kwa klabu ya Al-Ittihad kwa pauni ilioni 50. (Guardian)
0 Comments