MWENGE WA UHURU WAAGIZA UJENZI JENGO OFISI MPYA ZA MANISPAA SINGIDA UKAMILIKE

 

MWENGE wa Uhuru 2024 umeweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi mpya za Halmashauri ya Manispaa ya Singida na kuagiza ujenzi ukamilike kwa wakati ili huduma zianze kutolewa kwa wananchi.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2024,Godfrey Mnzava, akizungumza leo (Julai 8, 2024) baada ya kukagua mradi huo amesema muda wa nyongeza ambao amepewa mkandarasi anayejenga  ujenzi ukamilike ili wananchi waanze kupewa huduma katika ofisi hizo mpya.

Amesema serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya kiutawala ili wananchi wapate huduma kwenye maeneo mazuri lakini pia ilete heshima kwa ofisi za serikali zinakuwa na hadhi nzuri.

Mnzava amesema watumishi nao wakifanya kazi kwenye ofisi nzuri wanakuwa na furaha na amani wanapowahudumia wananchi na ndio maana serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu.       

Naye Mkuu wa Idara  ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Singida, Edward Mboya, akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo amesema Halmashauri ya Manispaa ya Singida ilipokea Sh. Bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Ofisi mpya za Manispaa kutokana na uchakavu wa jengo lilnalotumika kwa sasa na kushindwa kukidhi mahitaji yaliyopo. 

Amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 HAlmashauri ya Manispaa ilipokea Kiasi cha Sh. Bilioni moja kwa  ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa awamu ya kwanza na mwaka wa fedha wa 2023/2024 zilipokelewa Sh.bilioni moja utekelezaji wa ujenzi wa awamu ya pili. 

 Mboya amesema gharama za mradi hadi utakapokamilika itakuwa Sh.bilioni 3 ambapo hadi sasa kwa awamu zote mbili                          Sh. 1,982,707,354.08 kati ya Sh.Bilioni 2 zilizopokelewa  zimeshatumika na baadhi ya vifaa vya umaliziaji kama mabati na Gpysum vimeshanunuliwa na kuhifadhiwa katika stoo.

Amesema utekelezaji wa mradi huu umefanyika kwa awamu mbili, awamu ya kwanza inahusu ujenzi wa fremu ya jengo (Framed structure) pamoja na kuta na awamu ya pili ni umaliziaji na awamu ya pili kazi za ukamilishaji zinaendelea ikiwa ni pamoja na uwekaji wa mfumo wa maji, umeme na mifumo ya TEHAMA.

Mboya amesema faida ya mradi huu kwa wananchi kutoa huduma kwa wakaazi zaidi ya 200,000 wa Manispaa ya Singida na kuwezesha ajira za muda kwa makundi maalumu ya Vijana na Wanawake.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments