MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI CHUO WA UTUMISHI WA UMMA SINGIDA

 

MWENGE wa Uhuru kitaifa 2024 umeweka jiwe la msingi katika Chuo cha Utumishi wa Umma Singida kinachojengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey Mnzava, akizungumza leo (Julai 8, 2024) amesema Mwenge umeweka jiwe la msingi baada ya kupitia nyaraka za manunuzi yanayohusiana na ujenzi.

"Tumepata fursa ya kupitia nyaraka mbalimbali utekelezaji wa mradi jinsi ulivyofanyika tumeona namna ambavyo manunuzi yamefanyika,ubora wa vifaa ulivyopimwa na masuala yote ambayo yanahusu taratibu na kanuni za miradi ya maendeleo kama ambavyo imeelekezwa na serikali," amesema Mnzava.

Mnzava amesema maelekezo mahususi ambayo yametolewa na Mwenge wa Uhuru kwa viongozi yatekelezwe liliwako suala la wananchi ambao walichukuliwa maeneo yao wakati mradi unaanza kujengwa ijumuishwe kwenye maagizo ya utekelezaji.

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa chuo hicho, Afisa Raslimali Watu Chuo cha Utumishi wa Umma Singida, Martin Fute alisema ujenzi huu unafanyika kwa njia ya nguvu kazi (Force Account) kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha ambao ndio washauri elekezi na mafundi (Local Fundi) na kwamba utekelezaji wa mradi mpaka sasa umefikia asilimia 85.

Aliongeza kuwa chuo kinatekeleza mradi huu wa ujenzi kwa kutumia fedha za ndani na  kimetenga fedha kiasi cha Sh.bilioni 1.381 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu. "Mpaka sasa kampasi ya Singida imeshapokea  Sh.938,360,500) ambazo zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi, uwekaji wa miundombinu ya awali katika eneo la ujenzi, malipo ya kwanza ya mshauri elekezi na malipo ya kwanza ya mafundi na mradi unatarajia kukamilika 30 Septemba, 2024


Ameongeza kuwa faida za mradi ni kwamba utakiwezesha Chuo Cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Singida kuepuka gharama kubwa za kukodi majengo zinazofikia Sh.milioni 130 na wananchi wanaozunguka eneo la ujenzi wamepata fursa ya kutoa huduma mbalimbali kama vile chakula na hivyo kujiongezea kipato. 

Serikali na Wananchi wa Manispaa ya Singida  tunafurahi kuupokea Mwenge wa Uhuru, Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Waratibu wa Mwenge wa Uhuru kitaifa katika Kijiji hiki cha kisaki, Karibuni sana. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida,Godwin Gondwe, akitoa salamu wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Thomas Apson, amesema Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Singida utakimbizwa katika umbali wa kilometa 88 na utapitia miradi 7 ambapo mradi 01 utazinduliwa, miradi 03 itewekewa mawe ya msingi, na miradi 03 itatembelewa yote ikiwa na thamani ya Sh. 74,612,106,092.

Amesema miradi hiyo itajumuisha ya sekta ya Afya, Maji, Elimu, Mazingira, Miundombinu ya barabara na Maendeleo ya Jamii. 

"Pamoja na miradi hiyo, ndugu wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mtapata fursa ya kuona juhudi za Manispaa ya Singida katika kukabiliana na Malaria, virusi vya ukimwi (VVU) (Maambukizi mapya), Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Masuala ya Lishe na Mapambano dhidi ya Rushwa," amesema Gondwe.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments