MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka wakuu wa wilaya za mkoa huo kufanya ukaguzi wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato kila baada ya wiki katika halmashauri zao ili kuziba mianya yote ya upotevu wa fedha za Serikali zinazopatikana kupitia vyanzo mbalimbali.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu huyo wa mkoa wakati akikabidhi Magari mapya manne kwa wakuu wa wilaya za Kilindi, Pangani, Korogwe na lingine moja kwajili ya ufwatiliaji wa miradi ya maendeleo yaliyoghalimu kiasi cha shilingi Milion 683.
Mkoa wa Tanga katika mwaka wa fedha 2022/2023 umeweza kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato na hatimaye kufikisha asilimia 104 huku Wilaya ya Kilindi ikiwa Kinara katika halmashauri 11 za mkoa huo baada ya kukusanya kwa asilimia 131
"Niendelee kuwapongeza sana kama mkoa tumeweza kufanikiwa kukusanya mapato ya takribani asilimia 104 inaonyesha halmashauri zetu 5 zimekusanya na kuvuka lengo la asilimia 100 halmashauri zingine tunajua wanao uwezo wakaze buti wahakikishe wanasimamia wakusanyaji wa mapato "alisema dkt Buriani
Wakati huo huo Dkt Buriani amepongeza ufaulu mzuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2024 ambapo Mkoa umefanikiwa kutinga nafasi ya 10 Bora kupitia shule ya Sekondari Mkindi iliyopo wilayani Kilindi.
'"Huu ni mkoa ambao elimu ilianza hakuna sababu ya kuwa chini hapa tulipofika nina imani tunaweza kuwa na matokeo mazuri zaidi kwaajili ya kuendelea historia ya mkoa wetu wa Tanga"
Akizungumza Mwenyekiti wa wakuu wa wilaya za mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Hashimu Mgandilwa amesema ujio wa Magari hayo umeowaongezea ari ya utendaji kazi ambao itakwenda kutimiza adhima ya Serikali katika nyanja mbalimbali husausani kuwafikia wananchi kwa kutatua kero zao na kuwaleta maendeleo.
" Kwa niaba ya wenzangu niendelee kumpongeza na kumshukuru sana Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutukabidhi vitendea kazi hivi, tukuhakikishie vyombo hivi vya usafiri tutakwenda kuvitumia vizuri katika yale matarajio ambayo yeye binafsi anapenda yatokee kwa wananchi wetu hususani utatuzi wa migogoro na usimamizi wa miradi vitendea kazi hivi vimetutia chachu na kutuongezea ari ya ufanyaji wa kazi"alisema Mgandilwa.
Katibu wa chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Suleimani Sankwa amepongeza utendaji wa watumishi wote waliopo chini ya mkuu wa mkoa kwa kazi wanazoendelea kuzifanyia kwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ambayo imeongeza na kuchagiza maendeleo kuanzia ngazi ya vijiji na vitongoji na mitaa
0 Comments