Vilabu vya michezo lipeni ada ya ushiriki

ARUSHA: TAASISI na Mashirika ambayo yana malimbikizo ya ada za ushiriki wa michezo ya wafanyakazi zimeombwa kulipia ada ya ushiriki mapema ili kufanikisha michezo hiyo inayofanyika kila mwaka wakati wa Siku Kuu ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa Roselyne Mathew Massam kwenye kikao cha Viongozi Vilabu vya michezo ambvyo vipo kwenye Mashirikisho ya Michezo nchini ambao wamekutana kufanya tathimini ya michezo hiyo iliyofanyika mwezi Aprili mwaka huu Jijini Arusha.

SOMA: https://www.michezo.go.tz/

Massam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma (SHIMUTA), amesema kuwa ucheleweshaji wa ulipaji wa ada unakwamisha ufanisi wa michezo hiyo na kusababisha kushindwa kugharimia gharama za michezo hiyo ikiwemo kulipia viwanja vizuri vyenye ubora.

SOMA: Mashindano mei mosi kuanza Aprili 16 Morogoro

Naye Katibu Mkuu wa Kamati ya Michezo Taifa Alex Faustini Temba, ameishukuru Serikali kwa kutoa kibali kwa wafanyakazi kushiriki michezo hiyo ambapo mbali na kucheza michezo hiyo tofauti tofauti walichanga fedha shilingi milioni 13, ambazo walizitoa kwa Vituo vya wahutaji jijini Arusha.i.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments