Wafanyabiashara China washiriki Sabasaba

DAR ES SALAAM; WAFANYABIASHARA wa viwanda 25 vya China wapo nchini kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba mwaka 2024.

Mkurugenzi wa kampuni za usafirishaji mizigo za Kitanzania DM Mall na MMG Logistics, Hamid Idrissa Hamid, ambaye ameratibu ujio wa wafanyabiashara hao, amesema ujio wao ni kuonesha bidhaa wanazozalisha, kutengeneza mtandao na wafanyabiashara wa Tanzania,  lakini pia, kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuvutia wawekezaji.

Ametaja baadhi ya viwanda vya wafanyabiashara hao ambavyo vitaonesha bidhaa ni pamoja na nguo, vifaa vya nyumbani, simu, sola, viatu, mitambo, vinywaji, Jenereta, magari, vyakula, bidhaa za urembo na bidhaa mbalimbali, ambapo watatumia maonesho hayo kuuza na kuonesha shughuli zao.

“Lengo la kuwaleta hatutaki kikundi cha watu kinufaike peke yao bali tunataka Mtanzania mmoja mmoja anufaike, apate kitu kwa bei ndogo, ili kuvutia kampuni hizo kuwekeza nchini na kufungua viwanda na kutoa ajira nyingi kwa vijana,”amesema.

Meneja Masoko wa DM Mall na MMG Logistics, Haruna Said amesema baada ya kuona changamoto wanazopitia wafanyabiashara wa Kitanzania, vijana waliosoma China waliona kuna haja ya kuwasaidia wafanyabiashara kwa kuwaunganisha na kampuni za China kufanya biashara na kupata mizigo yao kwa wakati.

Amesema tangu wameanza ushirikiano na kampuni mbalimbali za Cjhina kwa zaidi ya miaka mitano wameajiri vijana zaidi ya 35 hapa nchini na China.

Amesema ujio wa wafanyabiashara hao ni kutaka kuonesha umakini kwa kutangaza bidhaa zao original zenye ubora zilizotoka katika miji tofauti ya China.

“Imezoeleka mtu anapoagiza mzigo wake kutoka China hufika Tanzania kwa kuchelewa, lakini kampuni zetu ni za uhakika katika kufikisha bidhaa kwa wakati,” amesema.

Miongoni mwa wafanyabiashara hao kutoka Kampuni ya XY Cargo Feler Logistics ya China, Xu Jian ameema wamechagua kuja Tanzania kwa kuwa ni sehemu salama kwa kufanya biashara, lakini pia wakitegemea kupata wateja wengi wa kushirikiana nao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments