Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
SERIKALI inatarajia kutumia zaidi ya Sh Bilioni 1.5 kwa ajili yakufanya maboresho ya sehemu za watu mashughuli (V.I.P lounge) katika viwanja vitatu vya ndege ambavyo ni uwanja wa ndege wa Mwanza,Arusha na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
Maboresho hayo ya maeneo ya watu mashughuli ni muendelezo wa uboreshaji wa viwanja hivyo yaliyoanzia katika Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kuzindua magari mawili aina ya Mercedes Benz E hundred yaliyonunuliwa na kampuni inayotoa huduma katika kiwanja cha ndege cha JNIA ya Swissport,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura amesema uboreshaji huo ni sehemu ya muendelezo ambapo mamlaka imejipanga kuweka mazingira mazuri yenye hadhi katika viwanja hivyo.
“Hapa JNIA tulishafanya marekebisho tangu Machi mwaka jana ambapo tulitumia Sh Milioni 600,hizi gharama zilijumlisha kila kitu ikiwemo kubadili eneo hili kulifanya lakisasa pamoja na kuweka samani za humu pamoja na kuweka huduma ya WIFI.
“Mwaka huu tumetengewa fedha kwa ajiili ya ukumbi wa uwanja wa ndege wa Mwanza,Arusha na Kilimanjaro kwa ajili yakuboresha kumbi zetu za VIP ambazo zitakuwa sawa na za Dar es Salaam bajeti,bajeti itategeemeana na maeneo ambapo bajeti yake inacheza kwenye Sh Milioni 500 mpaka 600,”amesema Mbura.
Amesema uboreshaji huo unatarajia kubadilisha kila kitu katika viwanja hivyo ndani ya eneo la watu mashughuli na kufanya ukumbi huo kuwa wa kisasa zaidi na kufanana na kumbi nyingine za duniani.
Amesema lengo la kuweka hadhi katika viwanja hivyo ambavyo vinapokea wageni wengi wakiwemo watalii ni kuongeza mapato ambayo yanapatikana kupitia huduma hiyo.
Amesema kwakuwa serikali teyari ilishafanya maboresho hayoambapo ilibaki nafasi ya wadau ambao wanatoa huduma hiyo ambapo kampuni ya Swissport imeanza kwakuleta magari yakupokelea wageni.
“ Sisi tulishafanya lakini Swissport kama wadau tunaoshirikiana nao walikuwa bado hawajaboresha kwakuweka kuweka vifaa ambavyo vingesaidia abiria wanaopita hapa kuweza kuwasaidia mojawapo ikiwa ni magari tukawaandikia barua na wakaleta mrejesho wa haraka .
“Tunaishukuru kampuni hii tayari wameshaleta magari haya mapya Mercedes Benz ambazo zitatumika ka watu wanaopita katika ukumbi wa watu mashughuli,”amesema Mbura.
Amesema uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha JNIA umeenda sambamba na kuongeza malipo yakupata huduma hiyo ambapo awali ilikuwa Sh 50,000 hadi Sh 100,000 lakini sasa lakini sasa itaanzia Sh 150,000 hadi Sh 250,000.
“Hii ni kwa sababu kuna watu hawapendi kuonekana wakiwa wanasafiri wapi wengine wanasafiri na ndege binafsi hivyo huduma hii itamfanya mtu akae mahali ametulia huku wahudumu wakimfanyia maandalizi ya safari yake,”amesema.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Swissport Mrisho Yassin amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa takribani miaka kumi uwanjani hapo ambapo wamekuwa wakishiriki katika maboresho mbalimbali kwakuleta magari tofauti tofauti.
“Leo tumezindua Mecedes Benz E hudred kwa ajili ya wateja wetu,magari haya yote mawili yana thamani ya Sh Milioni 700 fedha ambayo imejumlisha kodi zote za serikali tunaamini itasiadia kuboresha huduma tunazotoa katika eneo la VIP,”amesema.
0 Comments