Michezo hutoa fursa kwa vijana kustawisha
vipaji vyao, kupata mafunzo na uzoefu muhimu, na pia kujenga maadili na tabia
nzuri kama vile bidii, umoja na nidhamu.
Hata hivyo ni muhimu
kuzingatia kwamba michezo peke yake haiwezi kutimiza ndoto za vijana kama
haitawekewa misingi mizuri.
Kuna mambo mengine
muhimu kama vile elimu bora kwa kuzingatia mafunzo alioyapata na kuzingatia
uzalendo na mazingira mazuri ya kufanyia
mazoezi na kupata , ushauri na uongozi sahihi, pamoja na kuwa na nguvu ya
kuendelea licha ya changamoto mbalimbali zinazopatika katika kufanya kazi hiyo.
Kwa hivyo, ni muhimu
kuwa na mkakati wa pamoja na kamili
ambao unazingatia mambo yote hayo ili kustawisha ndoto za vijana katika soka na
michezo mingine na sio sehemu ya kuwa na watu wanao waza leo yao kuliko kesho
yake yenye mafanikio kwake na jamii kwa ujumla.
Serikali, mashirika
yasiyo ya kiserikali, wazazi na jamii nzima wanapaswa kushirikiana kuunda
mazingira rafiki kwa maendeleo ya vijana, na si mtu mmoja kuona anajua kuliko
wenzake.
Kwa ujumla, michezo ni
njia muhimu ya kustawisha ndoto za vijana ambao ndio uti wa mgongo wa jamii na
taifa ,lakini inahitaji kuwa na mkakati kamili na ushirikiano wa pande zote ili
kufanikiwa.
0 Comments