RAIS Samia Suluhu Hassan ametaka Tamasha la Kizimkazi kuwekwa kwenye orodha ya matamasha yanayotambulika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuwa miongoni mwa matamasha linalokuza utalii nchini.
Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Agosti 24 alipozungumza katika kilele cha kufunga tamasha hilo lililodumu kwa wiki moja katika uwanja wa Mwehe, Kusini Unguja, Zanzibar.
SOMA: PICHA: Rais Samia tamasha kizimkazi Zanzibar
Akizungumzia matukio yaliyofanyika katika tamasha hilo na mwelekezo wake, Rais Samia amesema kutokana na kukuwa kwa tamasha hilo wameamua kuanzisha taasisi maalum itakayosimamia na kuendesha shughuli zake.
“Kutokana na kukuwa kwa tamasha hili tumeamua kuanzisha taasisi maalum itakayosimamaia na kuendesha Tamasha la Kizimkazi,” amesema Rais Samia.
SOMA: Wizara ya Nishati yashiriki tamasha Kizimkazi Zanzibar
0 Comments