Tume ya Utumishi wa Mahakama imeweka Mkakati wa kuwafikia wananchi na kutoa elimu kuhusu uwepo wake, namna inavyotekeleza majukumu yake zikiwemo kamati zinazopokea malalamiko ya ukiukwaji wa maadili kwa Maafisa Mahakama na namna ya kuwasilisha malalamiko hayo.
Naibu Katibu (Maadili na Nidhamu) Tume ya Utumishi wa Mahakama ALESIA MBUYA alisema hayo mkoani Singida wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Tarafa wa mkoa hua kuhusu majukumu ya Tume hiyo ili waweze kwenda kuwaelimisha wananchi kuhusu Tume hiyo ya Utumishi wa Mahakama.
Alisema moja ya mikakati ya kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwaelimisha ni kwa kuwatumia Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Singida, lengo likiwa ni kuwaelimisha ili nao waende kuwaelimishe wananchi kupitia fursa walizonazo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa wananchi.
ALESIA alisema Tume imeona ni muhimu kuwatumia Maafisa Tarafa kuwaelimisha wananchi kuhusu uwepo wake na majukumu yake ikiwemo kuwaelimisha namna ya kuwasilisha malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa Maadili kwa Maafisa Mahakama kwa kuwa Maafisa Taarafa ni kiungo kati ya Serikali na Wananchi katika Tarafa, ni wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya katika shughuli mbalimbali za kijamii, Miradi ya Maendeleo na katika kutatua migogoro ya wananchi.
ALESIA pia alitoa wito kwa Maafisa Tarafa hao kuitangaza Tume ya Utumishi wa Mahakamana majukumu yake pale mnapopata nafasi ya kuisemea.
Hata hivyo aliwataka kuzingatia maadili ya Uongozi katika Utumishi wa Umma na kujiepusha na vitendo vya Rushwa kwa kuwa ni adui wa haki ili wawez kutenda haki kwa unaowaongoza.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Tume ya Utumishi wa Mahakama, LYDIA CHURI alisema Mafunzo haya yatasaidia kuwajengea uwezo ili wakaisaidie Tume kuwaelimisha Wananchi namna ya kuwasilisha Malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa Maadili ya Maafisa Mahakama na hatimaye wapate haki zao.
LYDIA alisema wananch hawana budi kufahamu namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa Tume hiyo ili waweze kupata haki zao, hivyo Tume ya Utumishi wa Mahakama iliona umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa Maafisa Tarafa ili waweze kutoa elimu hiyo kwa wananchi.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo walisema mafunzo hayo yatawasaidia kuwaelekeza wananchi kutatua changamoto zinazowakabili pale panapokuwa na ukiukwaji wa maadili na baadhi ya maafisa wa Mahakama.
Walisema pia mafunzo hayo yatawasaidia kufanya kazi kwa kufuata miongozo na kanunu za utumishi wa umma na hatimaye wananchi kupata huduma bora kuto kwao kama viongozi katika maeneo yao
0 Comments