UONGOZI WA MACHINJIO YA NGURU RANCH HILLS WAPONGEZA SERA ZA RAIS SAMIA KUWEZESHA UPATIKANAJI MASOKO YA KIMATAIFA

UONGOZI wa Machinjio ya Nguru Ranch Hills, umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Sera zake nzuri za biashara na uwekezaji, zilizopelekea ufanisi katika uendeshaji wa Machinjio hayo ya kisasa nchini.

Shukrani hizo zimetolewa na Meneje Mkuu wa Machinjio hayo, Bw. Eric Cormack, wakati Rais Samia alipotembeela banda la Nguru Hills Ranch, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Tutunzane, kwenye viwanja vya Sokoine Wilayani Mvomero Agosti 3, 2024.

Machinjio ya Nghuru Hills Ranch yanamilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na wabia wengine wawili, Eclipse Investment LLC kutoka Oman na Busara Investment LLP ya hapa nchini.

“Hizi zote ni juhudi zako kwenye Public Private Partnership, tunakushukuru sana kwa hilo na haya ni matunda ya wazi kabisa, juhudi zako zimesaidia kufungua masoko, wateja wetu wamekuwa wakitueleza,” alisema Bw. Cormack.

Aidha, Mhe. Rais Dkt. Samia, alipata fursa ya kuelezwa hatua kwa hatua za utekelezaji wa shughuli za Machinjio, kuanzia Ufugaji (Unenepeshaji mifugo), Uchinjaji, na Ufungashaji wa nyama kwa ajili ya usafirishaji kwenda kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.

Pia Bw. Cormack alimueleza Rais Samia kuwa Machinjio hayo yanafuata taratibu za Halal (Australia Halal Certification) hatua iliyosaidia kuaminika kwenye masoko ya nje hususan nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council-GCC), ambazo ni pamoja na Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia, na The United Arab Emirates.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa machinjio ya kisasa ya Nguru Hills, Bw. Eric Cormack juu ya uzalishaji wa bidhaa za nyama ambazo zinauzwa ndani na nje ya nchi, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Tutunzane, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro tarehe 03 Agosti, 2024. Machinjio hayo yanaendeshwa na PSSSF pamoja na wabia wengine.










TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments