UBINAFSI WA VIONGOZI WANAO SIMAMIA VILABU ,NIKIKWAZO CHA MAENDELEO YA SOKA BARANI AFRIKA


Ubinafsi wa viongozi wanao simamia vilabu na ukosefu wa wataalamu baadhi ya vilabu nikigezo kukubwa sana kinachepelekea kukwamisha maendeleo ya soka katika maeneo mbali mbali hapa nchini


Baathi ya Viongozi Barani Africa wamekuwa wakijitolea kuanzisha vilabu  mbali mbali ndani na nje ya nchi lakini vinaosimamiwa na viongozi wasio na ujuzi, uzoefu na utashi  wa kutosha katika usimamizi wa vilabu vya kisoka hii husababisha maamuzi yasiyozingatia maslahi ya klabu na wachezaji.

   

Viongozi wasio kuwa na weledi huanzisha vitu vingi visio kuwa nafaida kwa  timu na kusababisha   vilabu  hivyo kuonekana vimejengwa kwa madhumuni ya kibinafsi na ufisadi kuliko kuendeleza soka, na viongozi huiba fedha za klabu na kushindwa kuwekeza ipasavyo.

 

Ukosefu wa utawala bora, Mfumo duni wa utawala ndiyo kinachotawala mengi ya vilabu vya Afrika hakuna uwazi, uwajibikaji wala ushirikishwaji wa wadau muhimu.


Baadhi ya viongozi wasio kuwa na ujuzi huaribu malengo ya wamiliki wa vilabu kwa kutaka wao wathaminiwe sana kuliko kazi wanazofanya katika vilabu, na wakati mwingine wanafanya kazi ya kuwafelisha wanaofanya kazi vizuri ili wao waonekane wanafanya kazi.

 

Viongozi wasio kuwa na ujuzi katika soka husababisha ugumu wa kifedha,Vilabu vingi huwa na changamoto za mapato kidogo, hivyo kushindwa kuajiri wataalam na kulipa mishahara ya wachezaji wazuri.


Ili kuboresha hali, vilabu vinahitaji kuongozwa na viongozi wenye ujuzi, utashi weledi na azma ya kweli ya kuendeleza soka. 


Pia utawala bora, uwazi na kupambana na ufisadi ni muhimu. Serikali na washirika wa maendeleo wanapaswa kusaidia vilabu kiufadhili na ubunifu.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments