AJALI YAUA 12 MBEYA

 

Watu 12 wamefariki Dunia na wengine 23 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Septemba 27 Mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imetokea eneo la Jojo Kata ya Ilembo ikihusisha gari aina ya Fuso ambayo ilikuwa ikielekea kwenye soko kwa ajili ya mnada.

Mmoja wa mashuhuda katika eneo hilo, Elias Shiwiwi amesema gari hilo la Kampuni ya Chakazi likiwa limebeba wafanyabiashara kwa ajili ya mnada wa leo, lilikatika propela na kusababisha vifo kadhaa.

"Palepale wamefariki watano, baadaye wengine watano wakafia njiani wakielekea kituo cha afya Ilembo nikiwa nawaona hadi kufika kituoni hapo" amesema Shiwiwi.

Mganga mkuu wa kituo cha Afya Ilembo, Dk Philimon Irungi amethibitisha kupokea miili ya watu 11 ambapo mwingine mmoja alifariki baada ya kufika kituoni hapo.

"Eneo la tukio walifariki 11, ikatangulia miili sita kisha ikaja mitano na mmoja akafariki wakati akipatiwa matibabu, majeruhi ni 23" amesema Dk Urungi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments