RAIS DR. SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Bw. Salim Ramadhani Msangi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Msangi alikuwa akikaimu nafasi hiyo; na


Bw. Abdul Athumani Mombokaleo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mombokaleo alikuwa Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), anachukua nafasi ya Bw. Mussa Mbura ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments