VILABU TANZANIA VINAPASWA KUANZISHA VITENGO MAALUM VYA UCHUNGUZI KWA MASLAHI MAPANA YA MAENDELEO YA SOKA

Baadhi ya nchi na vyama vya soka vimeanzisha vitengo maalum vya uchunguzi wa ufisadi katika vilabu hii inalenga kuchunguza na kufuatilia malalamiko ya ufisadi ambapo imekuwa ni chanzo kikubwa cha migogoro mbali mbali hasa kwa wachezaji na vingozi wa vilabu husika.

 

Kwa upande wa vilabu kumekuwa na sitafaham kubwa hasa wakati wa usajili

Kwani baadha ya  vingozi na wachezaji wanaosajiliwa wamekuwa sio wakweli na mwisho wake wanaenda kuchafua taswila ya soka letu kwa maslahi yao binafsi

 

 

Kwa mfano katika ligi soka Tanzania Bara usajili wa Lameck Lawi  kutoka cost union kwenda Simba haukuwa na uwazi ndiomana  ukuzua migogoro kati ya simba na cost Union   kwa upande wa  Yusuph Kagoma  usajili wake umekuwa wa mvutano baada ya viongozi wa Yanga wakisema ni mchezaji wao na huku mchezaji akitumikia Simba, na kwa upande wa  Israel Mwenda kutoka Simba Kwenda Singida Black Sters bado kumekuwa na migogoro ambayo imepelekea mchezaji kushindwa kuripoti kambini,  hiyo ni mifano michache  tu kwa ligi soka Tanzania bara.

 

Ili kusajili kuna viongzi lazima wahusike kutoka pande zote mbili kutoka kwa wasimamizi wa mchezaji na kutoka kwa viongzi wa vilabu hivyo tunahitaji kufanya uchunguzi ili kuendelea kuboresha soka barani Afrika.

 

   

Kuimarisha sheria na kanuni ,Vyama vya soka vimefanya marekebisho ya sheria na kanuni zao ili kuimarisha utawala bora na uwajibikaji. Hii inajumuisha masharti mapya ya uwazi wa fedha na adhabu kali kwa ufisadi.

   

Ushirikiano na mamlaka za kudhibiti ufisadi, Kuna ushirikiano unaoendelea kati ya vyama vya soka na mamlaka za kudhibiti ufisadi katika baadhi ya nchi, Hii inarahisisha uchunguzi na uendeshaji wa kesi za ufisadi katika vilabu.

  

Mafunzo na uhamasishaji: Kampeni za elimu na uhamasishaji zinaendelea Kufanywa ili kuwahamasisha wadau wa soka, ikiwa ni pamoja na Kiongozi, wachezaji na mashabiki, kuhusu madhara ya ufisadi na Umuhimu wa utawala bora.

 

Kuanzisha mifumo ya uwazi wa fedha: Baadhi ya vilabu vimefanya hatua za kuanzisha mifumo ya uwazi wa fedha ambapo mapato na matumizi yao huwa wazi kwa umma na wadau wengine.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments