WAJUMBE ZAIDI YA 200 KUTOKA NCHI 80 WAKUTANA JIJINI ARUSHA KUJADILI NAMNA BORA YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango amefungua Jukwaa la 24 na Mkutano wa 35 na Kamati ya kudumu ya fedha ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi Afrika UNFCCC unaofanika  jijini Arusha wenye kauli mbiu ya "Kuongeza kasi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia ufadhili unaozingatia Jinsia." ambapo amesema Tanzania inachukuwa hatua madhubuti kuongeza sehemu ya uzalishaji wa nishati mbadala kupitia umeme wa maji, jotoardhi, upepo na nishati jua.

Akizungumza jijini Arusha Dkt.Mpango amesema kuwa kupitia mchango iliodhamiriwa kitaifa wa Tanzania imeweka mbele malengo ya kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama vijijini na mijini kutoka asilimia 86 na 67.7 mwaka 2020 hadi asilimia 100 ifikapo mwaka 2030 ambapo amesema uchafuzi wa mazingira kwa silimia kubwa husababishwa na matumizi ya kuni na mkaa na sababu kuu ya matatizo ya kiafya.

Aidha ameongeza kuwa, kutokana na matumizi ya nishati ya mimea imeonekana kuwa chanzo cha gesi chafuzi na uchafuzi wa mazingira ndani ya nyumba katika sehemu kubwa ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa kuzingatia hilo Tanzania imefanya ipishi safi kuwa agenda ya kitaifa kwa kupiga debe na kuratibu mpango wa kusaidia wanawake katika upikaji safi wa Afrika ambapo mpango huo umelenga kuyoa teknolojia ya kupikia safi Barani Afrika.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazinhira Dkt. Ashatu Kijaji amesema nchi ya Tanzania imejitoa katika kikabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia mipango na sera mbalimbali ikiwemo sera ya taifa ya mazingira ya mwaka 2021, Mpango mkuu wa mazingira wa kitaifa wa miaka ya mkakati kutoka 2022 hafi 2032 na serq ya taifa ya uchumi wa bluu ya mwaka 2024 .

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa ili kuboresha hatua za hali ya hewa ,Tanzania inatafuta ushirikiano na washirika wa maendeleo katika kuimarisha uimara wa hali ya hewa katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko, kukuza teknolijia za kupikia safi na nishati safi, kutekeleza usimamizi endelevu wa ardhi katika maeneo yaliyokabiliwa na maporomoko ya ardhi pamoja na kutekeleza mbinu endelevu za usimamizi wa takataka ngumu katika miji mikubwa.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga pamoja na kuwahakikishia usalama wa kutosha na upatikanaji wa huduma zote muhimu kwa washiriki wa jukwaa hilo na mkutano huo amesema mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo iliyokumbwa na athari za mabadiliko ya tabianchi 

Chanzo Matukio Daima Media

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments