KAZI INAENDELEA KWA VITENDO MKOANI SINGIDA .SIMIYU MANYARA,ARUSHA KUUNGA...

                       
Ukamilishwaji wa mradi wa ujenzi wa barabara wilayani Iramba kwa kiwango cha lami unategemewa kuwa chachu ya maendeleo kati ya Mikoa ya Arusha, Simiyu na Mkoa wa Singida katika nyanja zote za maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kufuatia Ujenzi wa barabara ya Kitukutu-Gumanga-Chemchem-Sibiti,sehemu ya kitukutu -Kinampanda yenye urefu wa kilometac7.7 kwa kiwango cha lami.

Akizungumza wakati akikagua mradi huo unaofadhiliwa kwa asilimia mia moja na serikali ya TanzaniaWaziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari,Mhe.Jerry Silaa, amesema ni wakati wa wakulima na wafanyabiashara kujibu kiu yao ya kupata masoko ya kuuza bidhaa zao zaufugaji, kilimo ikiwemo mahindi,alizeti,pamba na vitunguu pamoja na na biashara nyinginezo 

Mhe.Silaa amesisitiza kuwa utekelezaji wa mradi huo utarahisisha upatikanaji na ufikiwaji rahisi wa huduma za afya kwa wananchi wa mikoa hio kwa wakati wote kutokana na miundombinu bora ya barabara hiyo inayotarajiwa kukamilika Machi 2025 na sasa utekelezaji wake ukiwa asilimia 62.5

"Barabara hii inakwenda kukata kiu ya watanzania kutoka Maswa,Mkalama,Karatu na Meatu kuunganika na Wilaya ya mkalama,Iramba na maeneo mengine.Ni wakati wa wakulima kutumia vizuri ruzuku za pembejeo za kilimo na upatikanaji rahisi wa bidhaa zao za kilimo na ufugaji.alisema Mhe.Silaa

Mradi huo unagharimu kiasi cha Tsh 9.31bilioni ukitekelezwa na mkandarasi mzawa M/s Samota wa Tabora chini ya usimamizi wa TANROADS Singida ukihusisha kunyanyua tuta,tabaka la udongo mgumu,tabaka la simenti,tabaka la kokoto na mwishowe tabaka la lami nyepesi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments