NCHIMBI; STAKABADHI GHALANI NI SERA YA CCM.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema mfumo wa stakabadhi ghalani ni sera ya CCM kupitia Ilani yake ya mwaka 2020- 2025 ikiwa na lengo la kumlinda mkulima dhidi ya wafanyabiashara wanyonyaji. 

Amesema kabla ya kuanzishwa mfumo huo, wakulima wengi nchini walikuwa wakinyonywa kwa kuuza mazao yao chini ya bei halisi hali ambayo ilichangia  umasikini kwa mkulima. 

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mwandoya wilayani Meatu mkoani Simiyu, Balozi Nchimbi amesema mfumo huu umelenga kumlinda mkulima. 

"Habari ya stakabadhi ghalani ni sera ya CCM baada ya utafiti wa kina uliandaliwa na wataalamu mbalimbali ndani ya nchi yetu na sisi CCM tukaandaa Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2020- 2025.


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments