UBAYA UBWELA MWISHO UDUGU UMALA, YANGA YATAMBA

 

KLABU ya Yanga imeendelea kuwa mbabe kwa mpinzani wake mkubwa Simba Sc mara baada ya leo kupokea kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake, tumeshuhudia kandanda safi kutoka kwa timu zote mbele hasa kwa kucheza soka la kushambuliana kwa dhamu bila mafanikio katika kipindi cha kwanza na cha pili kabla ya Yanga kupata bao la ushindi kwenye mchezo huo.

Kipindi cha kwanza Simba ilipata nafasi ya wazi kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Leonel Ateba lakini mlinda lango machachari wa Yanga Djidji Diara kuokoa hatari hiyo na kuwafanya kuwa salama kwenye dakika hizo.

Mpaka kipindi cha kwanza kuisha mechi ilikuwa 0-0, licha ya nafasi nyingi kutengenezwa na nyota wa timu hizo mbili.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kwa dakika kadhaa za mchezo ambapo faida ya mabadiliko ilionekana kwa Yanga kwani ilimuingiza kiungo wao mshambuliaji Chama ambaye alitengeneza shambulio la hatari ambalo lilizaa bao kupitia kwa beki wa Simba Kijiri kujifunga akijaribu kuokoa.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments