BUNGE LARIDHIKA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MISITU NA NYUKI, LAIPONGEZA WIZARA

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhika na miradi mbalimbali ya misitu na nyuki inayotekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mfuko wa Misitu na Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora (BTI) na kupongeza kwa kazi nzuri inayofanyika.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Timotheo Mnzava (Mb) ametoa pongezi hizo leo katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Tabora wakati ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya misitu na nyuki huku akitaka juhudi hizo ziongeze ili kukamilisha kabisa kazi zilizobaki kwa baadhi ya miradi.

Kamati imefika jana ambapo inaendelea kesho kwa mkoa wa Tabora na Singida imeambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dustan Kitandula (Mb), Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi na baadhi ya Watendaji wa Wizara na taasisi zilizo chini ya Wiza


Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mheshimiwa Deusdedith Katwale pia ameipongeza na kuishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuleta ubunifu na wa kuanzisha nembo (trade mark) maalum inayotambulisha asali kimataifa.

“Napenda kuishukuru na kuipongeza Wizara ya Maliasili na utalii kwa mapinduzi makubwa kwenye sekta hii kwa kuanzisha nembo ya asali yetu ambayo itasaidia kuitambulisha asali ya Tanzania kwenye masoko ya kimataifa hivyo kuuza asali kwenye masoko ya kimataifa tofauti na awali.” Amefafanua Mhe. Katwale

Katika miradi hiyo Mfuko wa Misitu Tanzania umetoa ruzuku kwa miradi 56 katika Mkoa wa Tabora pekee yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 2.2

Miradi hiyo inatekelezwa katika Wilaya zote 7 za Mkoa wa Tabora ambazo ni Tabora, Uyui, Nzega, Igunga, Sikonge, Urambo na Kaliua.

Aidha, kati ya miradi hiyo ipo miradi ya ufugaji nyuki inayotekelezwa zaidi na vikundi vya kijamii, viwanda vya mazao ya nyuki na miradi ya kuimarisha Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora (BTI).

Pia Mfuko unagharamia ujenzi wa kiwanda na ununuzi wa mitambo kwa ajili mafunzo ya kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki katika Chuo cha BTI kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi. 

Kamati, pia imepata bahati ya kutembelea na kujionea mradi wa ukarabati wa jengo la utawala la Chuo, ujenzi wa jengo la karakana ya mbao kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa mafunzo ya utengenezaji wa mizinga bora ya nyuki, ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara (lecture theatre) kwa matumizi wanafunzi wa BTI na Kituo cha ufugaji nyuki kibiashara kilianzishwa kama mkakati wa kuongeza kipato cha jamii kwa uboreshaji wa uchumi na kupunguza uharibifu wa misitu ya hifadhi katika Mkoa wa Tabora.

Wakati huo huo Kamati imepata fursa ya kukagua mradi mkubwa wa ujenzi wa bweni la wasichana unatekelezwa katika Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora.

Mkuu wa chuo hicho, amefafanua mbele ya Kamati kuwa mradi huu umelenga kuongeza nafasi za malazi kwa wanafunzi wa kike, na hivyo kusaidia kuboresha elimu na usalama wao, ambapo kwa awamu ya kwanza bweni likikamilika litakuwa na uwezo wa kuwachukua wanafunzi 148.

Mradi huu unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia programu ya BEVAC, inayosimamiwa na Enabel kwa kushirikiana na Wizara ya maliasili na utalii ambapo gharama ya mradi ni takribani shilingi bilioni 2.6.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments