Mwalimu wa Karate wa Kimataifa mtanzania Sensei Rumadha Fundi anayetambuliwa na baraza ya Karate duniani ndiye mwafrika aliyealikwa
kuiwakilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla katika maadhiisho ya miaka 70 ya
baraza la karate Duniani huko OkinawaJapan. Gwiji mkongwe huyu Sensei Rumadha Fundi aliyebobea katika Sanaa ya Karate ana mkanda Mweusi (Black Belt) na Dan 6 ni miongoni mwa walimu nguli 300 kutoka kila kona duniani walialikwa huko Okinawa, Japan kuudhuria maadhimisho haya.
Leo hii siku muhimu sana katika historia ya chama cha karate cha Jundokan mtindo wa Okinawa Goju Ryu kuadhimisha miaka 70 tangu muasisi wa chama hicho master Eiichi Miyazato kuanzisha chama hicho huko mjini Naha, Okinawa, Japan.
Master Eiichi Miyazato ni mwanafunzi wa mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu, master Chojun Miyagi ambae aliunganisha sanaa ya Naha-Te na sanaa kadhaa za Kichina na kubuni mtindo huo wa Goju Ryu, ikimaanisha mtindo wa ngumu na laini.
Katika maadhimisho hayo,mwakilishi wa chama hicho cha Jundokan Tanzania, sensei Rumadha Fundi ambae kwa sasa yupo huko mjini Naha kuhudhuria maadhimisho hayo yanayo kusanyisha nchi zaidi ya 50 na washiriki masensei wapatao takribani 250 ikiwemo na Japan.
Kwa nchini Tanzania, Jundokan Karate ina matawi yake mikoa kama vile Dar es salaam,Morogoro, Dododma, Iringa, pia wapo wawakiishi toka Zanzibar, Moshi na Mwanza.
Uongozi wa Jundokan Tanzania na washauri wake chini ya jopo la masensei, Yusuf Kimvuli, Abdul-Wahid, Bilal Mlenga, Dr. Swai na kamati ya ushauri, Senpai Muhidin Issa Michuzi, Yahya Sameja na sensei Maulid Pambwe wanatoa pongezi kubwa kwa uongozi ulipo Okinawa kwa maadhimisho hayo ya kihistoria chini ya uongozi wa mwenyekiti Kancho Yoshihiro Miyazato.
Pia bila kusahau uongozi wa ngazi za awali toka kwa wanafunzi waandamizi Shabani Yusuf, Dodoma, Thobias Mgima, Mafinga, Iringa,nk. Kwa mujibu wa taarifa hii toka kwa sensei Rumadha Fundi, mafunzo muhimu ya kutumia zana za kujilinda KOBUDO pia itafundishwa katika maadhimisho hayo ya siku 7.
Lengo kuu pia ni kuwasahihisha walimu chini ya uongozi wa magwiji wa karate toka Okinawa,ni moja ya utamaduni wa mafunzo ya Karate hasa kwa chama cha Jundokan kuhudhuria huko Okinawa na kupata marekebisho sahihi ya mafunzo hayo. Alimalizia, sensei Rumadha Fundi.
0 Comments