WANANCHI SINGIDA WAPIGIENI KURA WAGOMBEA WA CCM ,NI CHAGUO SAHIHI- MWIGULU MCHEMBA

                             

Waziri wa Fedha Dr, Mwigulu Nchemba  na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM   amewahimiza Wanasingida na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 nchi nzima na kuwachagua wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi.


Amesema hayo leo (Jumanne, Novemba 26, 2024) wakati alipofunga kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizofanyika Wilayani Ikungi Mkoani Singida  

Amesema kwa kufanya hivyo ni kutimiza haki ya msingi katika kuwachagua viongozi watakaowatumikia katika kipindi cha miaka mitano “Huu ni wakati muhimu wa kufanya uchaguzi wa viongozi bora ambao wataleta maendeleo ya kweli, nendeni mkachague viongozi waliowekwa na CCM”

Amesema kuwa CCM inaamini kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho itawawezesha kuwa na viongozi wa kipekee, wanaojali na wanaohakikisha kuwa uwajibikaji na maendeleo vinapatikana kwa kila mwananchi.

“Hivyo basi, tutumie haki yetu ya kidemokrasia kwa kuchagua viongozi bora na kwa umoja kuhakikisha kuwa tunaendelea mbele kama taifa”

Na hizi ni picha mbali mbali katika mkutano huo






TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments