DKT.MATHAYO ATIMIZA AHADI ZAKE SAME AMWAGA MAMILIONI YA FEDHA KWENYE MIRADI

 Mbunge wa Same Magharibi, Mhe. David Mathayo,ameanza ziara ya siku sita katika jimbo la Same Magharibi na kuanza kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wananchi wake.


Akianzia kijiji cha Nasuro kata ya Mwembe Mathayo ametoa mifuko 100 ya saruji ya kujenga nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Nasuro, shilingi 1,760,000 kwa ajili ya madirisha ya nyumba ya mwalimu pamoja na mabati hamsini ya nyumba hiyo.

Pia, Mhe. Mathayo amekabidhi shilingi 2,000,000 kwa ajili ya milango ya nyumba hiyo ya mwalimu, shilingi 350,000 kwa ajili ya kununua kipimo cha Zahanati, shilingi 400,000 kwa ajili ya pumpu ya kumwagilia bustani ya mbogamboga ya kikundi cha vijana.

Akikabidhi msaada huo mhe.Mathayo amesema fedha hizo ni za kwake na ameamua kuwapunguzia wananchi mzigo wa kuchangishwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

“Mimi kama mbunge wenu nimekuja kutekeleza ahadi zangu zote nilizoahidi mara baada ya kuchaguliwa,heshima ya kiongozi ni huduma yake kwa umma tunajua vipato vyetu sio vingi kwa hiyo sisi viongozi kama wabunge tunapojitolea hivi kusaidiana kwenye shughuli za maendeleo maana yake tunapunguza gharama kubwa ambazo pengine wananchi wangechangia”,Alisema Mathayo

Alisema msaada hu oni kuuunga mkono juhudi za serikali chini ya Rais dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wapiga kura wake wa jimbo la Same Magharibi wanaondokana na adha mbalimbali,
“Fedha hizi nazitoa sio za serikali ni za kwangu kama mbunge kwa sababu sitaki wananchi wangu wasumbuliwe na michango ya mara kwa mara”.Alisema Mathayo

Mwenyekiti wa CCM kata ya Bangalala amemshukuru Mheshimiwa Mathayo kwa kutekeleza ilani ya CCM ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

Nae Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nasuro Upendo Emmanuel amesema msaada huo umekuja kwa wakati kwani utasaiida kupunguza changamoto ya ukosefu wa nyumba za walimu katika kijiji hicho lakini pia itawaondolea usumbufu wazazi wa kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.

Wananchi nao wammeshukuru mheshimiwa Mathayo kwa kutekeleza ahadi na kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo kwa kuwajenge miradi mbalimbali lakini pia kuwawezesha wanawake na vijana kujiajiri.
 

Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dkt.David Mathayo akikabidhi mabati 50  kwa ajili ya kununua milango na madirisha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Nasuro kata ya Mwembe .
 

Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dkt.David Mathayo akikabidhi fedha taslimu kwa ajili ya kununua milango na madirisha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Nasuro kata ya Mwembe .
 

Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dkt.David Mathayo akikabidhi mifuko mia moja 100 ya saruji kwa Viongozi wa kata ya Same na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Nasuro kata ya Mwembe .
 

Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dkt.David Mathayo akizungumza na Viongozi wa kata ya Same na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Nasuro kata ya  Mwembe .

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments