
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi JOSHUA MBWANA amewashukuru wananchi wa Wilaya hiyo kwa kukiamini Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuwachagua viongozi wengi wanaotokana na CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27. 11. 2024.
MBWANA alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wilayani humo akisema kuwa CCM imeshinda Vijiji na Vitongoji vingi ikilinganishwa na Chaguzi zilizopita.
Alisema Wilaya ya Ikungi ina Kata 28, Vijiji 101 na Vitongoji 539, na katika uchaguzi huo CCM ilishinda vitongoji 536 na upinzani kuambulia Vitongoji viwili (2).
MBWANA alisema katika Uchaguzi huo wa serikali za Mitaa kitongoji kimoja hakikufanya uchaguzi kufuatia mgombea wa Chadema kufariki siku mbili kabla ya uchagu baada ya kupata ajali ya Pikipiki.
Aiongeza kuwa katika Kata na Kijiji anachotaka Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chama cha Mapinduzi kimeshinda nafasi zote za Uongozi, hakuna hata Kiti kimoja kimeenda upinzani.
SABABU ZA CCM KUSHINDA VITONGOJI VINGI.
MBWANA alisema sababu kubwa ya CCM kufanya vizuri katika Uchaguzi huo ni kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN ya kuwapelekea wananchi maendeleo.
Alisema changamoto nyingi za wananchi zimetatuliwa na Serikali kupitia Miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika maeneo ya wananchi na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa huduma mbali.
Pia alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN wilaya ya Ikungi imepokea Fedha nyingi ambazo zimetumika kutatua changamoto za Wananchi kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na Sekta ya Elimu, Afya, Barabara na Kilimo.
Aidha aliongeza kuwa kwa sasa Wananchi wamekiamini Chama cha Mapinduzi kutokana kazi kubwa iliyofanywa na serikali, na ndio sababu kubwa ya wagombea wengi wa CCM kuibuka washindi.
MBWANA alisema wananchi kwa sasa hawataki maneno maneno tuu wanataka kuona vitendo, hivyo kutokana na kazi nzuri inayofanywa CCM, hawana mpango wa kuwapa kura vyama vyenye maneno ambayo hayana matokeo.
Hivyo amewataka wananchi waendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi katika Chaguzi mbalimbali zijazo ili waweze kupata viongozi ambao wataweza kutatua changamoto zao.
0 Comments