WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameshuhudia makabidhiano ya matrekta matano kati ya Wizara ya Kilimo na Halmashauriya Wilaya ya Ruangwa.
Makabidhiano hayo ni utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango wa serikali wa kukabidhi zana za kilimo kwenye vituo 45 vya zana nchini.
Majaliwa aliwataka wananchi watakaopata fursa ya kutumia matrekta hayo wayatunze yadumu kwa muda mrefu ili kuleta tija na kutimiza malengo yaliyokusudiwa “Tuna uzoefu wa matrekta tuliyoyaleta kipindi cha nyuma, hayakudumu kwa kuwa baadhi yetu tulikuwa tunayatumia kulima kwenye visiki, hii sio sawa, yatunzeni ili yale malengo tuliyoyakusudia ya kuendeleza sekta ya kilimo yatimie,” alisema.
Majaliwa alisema serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeandaa mpango wa kuhi[1]fadhi maji yanayotiririka katika mabonde ya Mpumbe, Nanguruwe, Mnindu na lililopo eneo la Lucas Maliaili yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dk Hussein Mohamed Omary alisema ugawaji wa matrekta hayo ni maelekezo ya Rais kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo ili kuongeza tija kwa wakulima.
Omary alisema katika awamu hiyo ya kwanza kwa Wilaya ya Ruangwa wamekabidhi matrekta matano, majembe matano ya kulimia, vifaa vya kuchimbia na kusafisha mashamba na kifaa cha kuvunia mazao.
Alisema katika awamu ya kwanza ya mpango huo Wizara ya Kilimo itaanzisha vituo 45.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma alisema matrekta hayo yatasaidia kuongeza eneo la kilimo hadi kufikia asilimia zaidi ya 50 kutoka chini ya asilimia 80 ya sasa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya alimshukuru, Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo.
0 Comments