MONGELLA AONGOZA KUAGA WANNE WA AJALI YA MBEYA

                      
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, leo tarehe 27 Februari 2025 ameongoza shughuli ya kuaga miili ya marehemu wanne waliopoteza maisha katika ajali ya gari wakati wakitokea kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Maganya, mkoani Mbeya.

Akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Mongella amesema chama kimetoa ubani  wa shilingi milioni 20 kwa familia za marehemu na shilingi milioni 6 kwa majeruhi sita wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Mongella ametoa pole kwa familia za marehemu na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu. 

Shughuli ya kuaga miili ya marehemu hao  imefanyika katika Viwanja vya Soko la Uhindini, jijini Mbeya.

                             




TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments