
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Azam uliokuwa umepangwa kufanyika uwanja wa KMC sasa utafanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Simba itakuwa mwenyeji wa Azam kwenye mchezo huo wa ‘Mzizima Derby’ Februari 24 jioni.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesema sababu ya mabadiliko hayo ni kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo ambao ni moja ya michezo mikubwa ya Ligi Kuu bara inayovuta hisia za watu wengi.
Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 umekuwa ukitumika kwa michezo mingi mikubwa na inayohusisha mashabiki wengi zaidi.
Simba ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 50 baada ya michezo 19 wakati Azam ni ya tatu ikikusanya pointi 43 baada ya michezo 20.
0 Comments