RAIS MWINYI AFUNGUA TRACE AWARDS 2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema   Serikali itaendelea  kuwaunga Mkono  Wasanii kwani ni  Muhimu katika Kukuza Utalii, Uwekezaji na Urithi wa Utamaduni miongoni mwa Jamii. 


Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipolifungua  Tamasha la Tuzo za Muziki la Trace Awards kwa mwaka 2025 linalofanyika  Hoteli ya The Mora ,Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja .

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Sanaa ya Muziki ina nguvu kubwa ya kuiunganisha jamii  na nyenzo muhimu ya kuchochea Ukuaji wa Uchumi , Uwekezaji na Ubunifu pamoja na kuibua Vipaji vya Vijana katika Sanaa.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametoa rai kwa Waandaaji na Washiriki wa  Tamasha  hilo  mbali na Kufurahia Muziki bali pia litumike kujenga Ushirikiano, Umoja na  Mahusiano mazuri miongoni mwa Wasanii 

Ameupongeza Uongozi wa Taasisi ya Trace Award kwa kuamua Tamasha hilo kufanyika Zanzibar kwa mara ya Kwanza kwani litaitangaza Zanzibar Kimataifa  pamoja na  Kukuza Utalii na kubainisha fursa za Uwekezaji na Utamaduni.

 Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza  Wadau na Wafadhili mbalimbali kwa kufanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo na kuahidi kuwa Serikali kuendelea  kuweka Mazingira bora zaidi Kwa Wasanii na kazi za sanaa kwa lengo la Kukuza  Vipaji vya Vijana, fursa za Ajira na Urithi wa Utamaduni.




 









TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments