Samia asikitishwa kifo cha Sam Nujoma

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kifo cha Rais Muasisi wa Taifa la Namibia, Dk Sam Nujoma kilichotokea jana usiku akiwa amelazwa hospitalini.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rais Samia ameandika: “Mpigania uhuru, Pan-Africanist na rafiki mpendwa wa Tanzania ambako aliwahi kuishi wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Namibia, Dk. Nujoma aliishi maisha ya utumishi ambayo yalitengeneza sio tu hatima ya nchi yake, bali pia kuhamasisha vizazi kusimama kwa ajili ya maadili ya uhuru, usawa na haki.

“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kuwasilisha salamu zetu za rambirambi kwa Mheshimiwa Dkt. Nangolo Mbumba, Rais wa Jamhuri ya Namibia, wananchi wa Namibia, Mke wa Rais Mwanzilishi wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Kovambo Nujoma, watoto wa Dk. Nujoma, familia yake yote, marafiki na wandugu wa SWA”. Ameandika Rais Samia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments