Serikali yapewa mwezi mmoja kukamilisha ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imetoa agizo kwa serikali kuhakikisha ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa unakamilika ifikapo Aprili 2025, ili uweze kukidhi viwango vya kimataifa kwa ajili ya mashindano ya CHAN na AFCON 2027.

Azimio hili limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Husna Sekiboko, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2024 hadi 2025, katika kikao cha Bunge kilichofanyika leo Februari 11, 2025 jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine, Sekiboko aliipongeza serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongezea bajeti wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Habari, Utamaduni na Michezo, jambo lililosaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi mingi kwa ufanisi.

Hata hivyo Sekiboko , aliiomba serikali kuhakikisha inatekeleza miradi inayoendelea kwa wakati ili kuleta maendeleo ya haraka kwa Taifa na Jamii kwa ujumla.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments