Serikali yathibitisha misaada ya Marekani kusitishwa.

DODOMA : WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameelezea msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu mabadiliko ya sera za misaada ya Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump, akisisitiza kuwa Tanzania inatakiwa kujikite katika kujitegemea kiuchumi.

Akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, George Mwanisongole, Bungeni jijini Dodoma, Majaliwa alisema kuwa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) imesitisha baadhi ya misaada kwa Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea.

Alisema kuwa mabadiliko haya ni sehemu ya sera mpya za mambo ya nje za Marekani, ambazo zinaweza kuwa na athari kwa baadhi ya sekta nchini.

“Ni kweli kwamba Serikali yetu inaheshimu sera za mambo ya nje na tunatekeleza mikataba kwa mujibu wa makubaliano na nchi husika. Hata hivyo, tumeanza kuona mabadiliko katika sera za baadhi ya nchi zenye uwezo mkubwa kama Marekani, na haya mabadiliko yanaweza kuathiri baadhi ya nchi, ikiwemo Tanzania,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha, Majaliwa alisisitiza kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha uchumi wake unajitegemea ili kuepuka utegemezi wa misaada ya nje. SOMA: Bunge lampongeza Samia mkutano wa nishati Dar

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments