Vijana Wanatuonesha Njia Tuwape nguvu Wafikie Malengo Rais Samia Suluhu

 Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk  Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ni wakati sasa wa vijana wa Afrika  kuongezewa nguvu katika uzalishaji wa zao la Kahawa  ili Malengo ya uzalishaji katika sekta ya kahawa  yafikiwe.

Rais Samia amesema hayo wakati akitembelea mabanda ya maonesho kwenye viwanja vya Ukumbi wa Mikutano ya  Kimataifa wa Julius Nyerere(JNICC), na wakati akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la nchi 25 zinazolima Kahawa barani Afrika mjini Dar es salaam 

Akilenga uongezaji wa thamani wa zao la Kahawa amesema utaongeza thamani ya zao hilo, kwani kwa sasa zao hilo linauzwa likiwa ghafi.na wanaonufaika ni  walewanaolinunua , wanapata faida mara mbili zaidi ya mkulima ambaye amelima nakufanya kazi kubwa.

Rais Samia amesema Tanzania iko tayari kufundisha vijana wa Africa Kilimo kwani tayari Tanzania inayo programu  ya BBT  inayolenga kuwawezesha vijana  kujiajiri . Ambapo Tanzania imejikita katika Kilimo ufugaji na uvuvi.

Kwa habari ya soko la kahawa Rais Samia amesema Azimio la Biashara huru kwa Afrika lazima lisimamiwe   vizuri "soko la Kahawa ilivyo kwa sasa ambayo ni kuuza Kahawa ghafi kwa bei ndogo Kisha inarudishwa  Afrika ikiwa imepakiwa na kuuzwa kwa bei kubwa . Tanzania imeanza  kupaki Kahawa ila ni vyema Afrika ikaungana kuhusu hili."

Ametoa Rai kwa nchi za Afrika kulejesha hadhi ya zao la Kahawa na kuzitaka zikubaliane naye kuwa ifikapo 2035 asilimia 50 ya zao la Kahawa liongezewe thamani  barani Afrika  liuzwe likiwa limesindikwa.











TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments